Makamuwa Pili wa Rais zanzibar- kumuwakilisha Rais wa Zanzibar- Tamasha la Kilimo hai- dole

 

Na, Fatma Rajab

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema kufanyika kwa Tamasha la Kilimo hai ni hatua moja wapo ya kuelekea kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, ambayo inalenga kuwa na maisha bora, endelevu na yenye ustahmilivu kwa Wazanzibari wote.

Ayamesemwa hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Mwinyi katika Tamasha la Kilimo hai la Mwaka 2024 lililofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nanenane Dole Wilaya ya Magharibi “ A” Unguja.

Amesema kuwa kufanyika kwa Tamasha hilo hapa Nchini kunapelekea kuwa na Utalii endelevu, kilimo cha asili, ustahamilivu wa hali ya hewa na kufikia malengo ya Kitaifa na dhamira ya Ulimwengu kwa  Maendeleo endelevu.(SDGs)

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema dhamira ya kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha Utalii endelevu na kilimo hai imeanza kuzaa matunda ambapo jitihada mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa ili kukuza uchumi na kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha Mhe.Hemed amesema kilimo hai ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula, kuimarisha Afya na kulinda mazingira kwa kuiwezesha jamii kupata vyanzo vipya vya maisha pamoja na kuimarisha ustahmilivu wa mifumo ya kilimo dhidi ya mabadiliko ya Tabianchi.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka kipaombele katika mipango inayounga mkono mbinu mpya za kilimo hai, kuanzia kilimo hadi utengenezaji wa bidhaa za kilimo hai zinazoongeza thamani kwenye uchumi wa Zanzibar.

Nae Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo inajipanga kufanya jitihada za hali ya juu kwa kuwashajihisha wakulima na wananchi kwa ujumla kufanya Kilimo hai chenye kupunguza matumizi ya viatilifu sumu, kulinda mazingira na kuimarisha Afya ya Mlaji.



Shamata amesema Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha Tamasha la kilimo hai linaleta Tija kwa kuongezeka kwa Chakula na kukua kwa uchumi kupitia Sekta ya Kilimo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kilimo hai Tanzania Dkt. Mwatima Abdalla Juma amesema Kilimo hai kinazidi kukuwa kwa kasi Duniani ambapo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo wameweza kuandaa Mkakati wa Kilimo hai Afrika na kutoa nafasi kwa nchi mbali mbali kuja kujifunza Tanzani  mbinu na mipango ya kuendeleza Kilimo hai.

Dkt. Mwatima amesema chamgamoto kubwa katika kuendeleza Kilimo hai Tanzania inatokana na kuendeleza matumizi ya Viatilifu sumu katika Kilimo ambavyo vinachangia kuongezeka kwa maradhi mbali mbali nchini, hivyo ameiomba Serikali kusimamia kuondoka kwa viatilifu sumu  ili kuendeleza dhana ya kilimo hai nchini.

Aidha Dkt. Mwatima ameiomba serikali kuwapatiwa ruzuku kwa ajili ya kilimo hai ambayo itatumika kwa kuwasaidia vijana kufanya utafiti utakao ibua mbinu mbali mbali za kuimarisha kilimo hai  sambamba  kuiomba Serikali kuridhia Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA) kuwa kitovu cha Kilimo hai hapa Zanzibar.

Mapema Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Kilimo hai Zanzibar Ikram Ramadhan soraga amesema lengo la Tamasha la kilimo hai ni kuweka msingi wa maendeleo endelevu pamoja na kukuza uwelewa kwa jamii juu ya kukuza mbinu mpya za kilimo hai Zanzibar.

Soraga amesema Tamasha la Kilimo hai linatoa fursa ya kuwaunganisha pamoja wakulima nchini pamoja na kuwatafutia soko ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha kilimo na kukuza utalii Zanzibar.

Mapema mkamu wa pili wa rais wa zanzibar ametembelea mabanda ya wajasiriamali,taasisi za serikali na binafsi pamoja na kujionesha shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi hizo.




Ubalozi wa Marekani kushirikiana Kibiashara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

 

NA FATMA RAJAB



Zanzibar, imejikita kwenye kilimo cha biashara kama mwani, viungo na Ujasiriamali ambao umewajumuisha zaidi  wanawake wanao jishughulisha na utengenezaji wa mafuta ya mimea, sabuni, utengenezaji vitambaa na sanaa za mikono

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma Mabrouk Khamis ameyasema hayo katika mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael A. Battle akiambatana na Maafisa biashara kutoka Ubalozi wa Marekani kwa lengo la kujitambulisha na kufanya mazungumzo ya kuimarisha Mashirikiano ya Kibiashara kati ya Marekani na Tanzania kwa upande wa Zanzibar.

Mazungumzo hayo, yamefanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Maruhubi, ambapo Bi Fatma amefafanua pande zote mbili zimekubaliana kuwa na mpango wa kuandaa eneo la kibiashara ambalo litaleta tija.

Aidha mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uvuvi kutokana na  Zanzibar kuwa na  eneo kubwa la Uvuvi wa baharini  (Deep sea fishing) linalohitaji kuimarishwa zaidi.

Kwa upande wa Ubalozi wa Marekeani wamesema kuwa wapo tayari kushirikiana na Zanzibar  kutoa Misaada ya kitaalamu pale inapohitajika ili kuisaidia Zanzibar kufikia katika soko la AGOA na masoko mengine kutokana na Zanzibar inatambulika ulimwenguni kwa biashara ya Utalii.

mazungumzo hayo ya siku moja yameangalia maeneo muhimu ya kibishara ambayo ni pamoja na uchumi wa kidijitali (digital economy), Mabadiliko ya Sheria katika Biashara, upatikanaji wa Masoko na kuanzishwa misafara ya Kibiashara.

 

 

 

 

Mhe, Hemed azindua Tathimin ya Mwisho ya PSSN II ya Mpango wa kunusuru kaya Masikin.

 

Na. Asia Makame



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeanzisha  mpango wa kunusuru Kaya Masikini (PSSN II) ili kupunguza umasikini uliokisiri katika Kaya mbali mbali Tanzania Bara na Zanzibar.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tathmini ya mwisho ya kupima matokeo ya mpango wa kunusuru kaya masikini kipindi cha pili ( PSSN II )Tanzania katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Amesema Mpango huo unaotekelezwa ndani ya Awamu ya Tatu ya TASAF  unalenga kuziwezesha kaya zinazoishi katika umasikini uliokithiri kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu na kuondokana na umasikini kwa kuimarisha uchumi wao kwa faida ya vizazi vijavyo na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Hemed amesema kaya za walengwa hupatiwa ruzuku ya msingi pamoja na mafunzo ya stadi za ujasiriamali na mbinu za kuunda vikundi endelevu vya kuwekeza katika shuguli mbali mbali za kiuchumi ikiwemo kilimo na biashara

Aidha Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa  kaya za walengwa hunufaika na fursa za ajira za muda mfupi na kujipatia kipato kwa kushiriki katika miradi mbali mbali ya maendeleo katika jamii kwa lengo la kuhakikisha  wanawasimamia vyema watoto wao katika kupata elimu na afya bora ili kujenga ustawi mzuri wa familia zao

Sambamba na hayo Mhe.Hemed amesema kuanzia mwaka 2000 hadi mwezi Agast 2024 Serikali imeweza kuzisaidia kaya za walengwa wapatao 1,450,000 ambao wameweza kujikwamua kutoka katika hali ya umasikini uliokithiri na kuweza kujitegemea kimaisha

Mhe. Hemed amezitaka Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar na Afisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania kuhakikisha Tathmini inayofanywa inatoa Takwimu zenye ubora  zitakazoonesha taswira halisi ya hali ilivyo na kuisaidia  Serikali kuona maeneo ambayo yamefanya vizuri zaidi na maeneo ambayo yanahitaji kuongezewa mkazo ili malengo ya TASAF yaweze kutimia



Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratib na Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Mhe. ALI SULEIMAN MREMBO amesema Serikali zimeweka mazingira mazuri ya kuhakikisha Mradi wa kunusuru kaya masikini unafanyika kwa ustadi na uweledi wa hali ya juu na kutoa matokea chanya yatakayowanufaisha Watanzania Wengi kwa kuwakwamua katika mazingira ya umasikini uliokithiri kwa baadhi ya kaya.

Mhe. Mrembo amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya Masheha na wananchi kutoa ushirikiano wakati wa kufanyika kwa zoezi la Tathmini ili kuweza kupata Takwimu sahihi zitakazo iwezesha Serikali kujipanga zaidi katika kuendelea na utekelezaji wa mpango wa  kuzinusuru kaya masikini Tanzania nzima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji kutoka TASAF Bwana Shedrack Mziray amesema madhumuni ya Kufanyika kwa Tathmini hio ni kuangalia ni kwa kiwango gani Serikali imeweza kuwasaidia wananchi wake kupitia uwekezaji ilioufanya katika Mpango wa Kunusuru kaya masikini Tanzania.

Amesema kupitia mpango huo miradi Elfu 27 imetekelezwa ikiwemo ajira za muda, kuanzisha vikundi vya kukopa na kuweka hakiba na kupatiwa mafunzo kwa wajasiri amali ambayo imewanufaisha zaidi ya  walengwa wapatao 662, 374 kwa pande zote za Muungano.

Mapema Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zanzibar Ndugu Salum Kassim Ali amesema kuwa utafiti huu unatarajiwa kufanyika katika Mikoa kumi na saba (17 ) kwa Tanzania nzima ili kufanikisha lengo la Serikali la kuwatatulia changamoto wananchi wa kaya masikini zilizopo nchini Sambamba na kuhakikisha tathmini hii itafanyika kwa kiwango kilichobora na kinachokubalika kitaifa na kimataifa.


Wananchi watakiwa Kufuata Sheria Sahihi Za Matumizi ya Ardhi

 

Na, Fatma Rajab



Wananchi wametakiwa kua na matumizi  mzuri ya Ardhi ili waweze kuepukana na changamoto mbali mbali ambazo zinaweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na waziri wa ardhi na maendeleo ya makaazi Mhe, Rahma Kassim Ali katika Ghafla ya uzinduzi wa utoaji hati miliki za Ardhi za kilimo (eka tatu)  iliofanyika katika ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.

Alisema ni vyema kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka husika pindi wanapotaka kubadilisha mashamba yao kutoka kwenye matumizi ya kilimo na kwenda kwenye matumizi ya makaazi ili kuweza kupata mabadiliko ya hekta yaliokuwa sahihi.

Aidha alisema, anawatak wananchi kuacha tabia ya kukata na kuuza maeneo  bila ya kufuata taratibu wakati wa kukatiwa viwanja hivyo na serikali kuchukuwa asiimia ndogo lengo ikiwa ni kuwashajihisha wananchi kuacha tabia ya kubadilisha matumizi binafsi na kuweza kuepusha matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake katibu mtendaji kutoka kamisheni ya Ardhi Mussa Kombo Hamad. alisema baada ya muda mrefu kutokuwepo kwa zoezi la utoaji wa hati miliki sasa wameamua kutoahati hizo zenye lengo la kuhamasisha wananchi mbali mbali wanaomiliki mashamba ya eka tatu kukamilisha taratibu za kupatiwa hati ya matumizi ya mashamba yalio sahihi.

Aidha alisema wanampngo wa kuendesha zoezi la kuhakiki maeneo ambayo yanafaa kuwa ni ya heka na kujua ni  mashamba gani ambayo yamepotea kuwa ni mashamba ya eka

"Tunafahamu kwamba hili ni zoezi muhimu na kwasababu ya umuhimu wa ardhi   kwa ajili ya kilimo na jambo ambalo limeasisiwa toka mapinduzi hivyo ni vyema kuliendeleza na kusimamia vizuri mashamba hayo ili yaweze kudumu kwa vizazi vya sas na baadae"

Aidha,aliwataka wananchi wenye mashamba ya kilimo ya Serikali wafike kamisheni ya Ardhi ili kuweza kupatiwa hati zilizo Rasmi ambazo zitasaidia kuondosha migogoro mbali mbali inayoweza kujitokeza.

Kwa Upande wao wananchi waliokabidhiwa hati hizo  walisema  wanaishukuru serikali kwa kuwapatia nyaraka hizo kwani kumepunguza changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zikijitokeza.

Hivyo ni vyema wananchi kufuata taratibu zilizowekwa kwa Ardhi ni mali ya watu wote na ni vyema kuitunza ili iweze kudumu kwa vizazi vya sas na vijavyo na zoezi hilo lilo ambatana na hati miliki ambazo ni halali kwa wananchi.

Serikali kuendelea kushirikiana Katika Miradi ya Kimakati

 



Na, Fatma Rajab



Serikali ya  SMT na  SMZ zitaendelea na juhudi za kuimarisha dhana ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa pande zote mbili za Muungano hasa katika shughuli za Mipango ya Kitaifa na Miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Hayo yamesemwa na na Mkamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifungua Kongamano  la Tatu(3) la Kitaifa la wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Mwinyi liliofanyika katika Ukumbi wa Hotel  ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar

Amesem Tanzania inaendele kupiga hatua katika uimarishaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini ikiwemo kuweka mifumo na miundombinu yenye kuwezesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo  kwa Taasisi za Kitaifa zinazoratibu masuala hayo kwa maslahi mapana ya nchini

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed amesema matumizi ya Teknoloji katika kufanya ufuatiliaji na Tathmini kutaiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuimarisha uwajibikaji  na kuongeza kasi na uwazi katika kuleta ustawi wa wananchi kwa kutoa huduma sahihi za kijamii na kiuchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa  anatambua kuwa mafanikio makubwa yamepatika katika shuhuli za ufuatiliaji na tathmini nchini hivyo amezitaka Mamlaka husika kufanya jitihada za kukamilisha maandalizi ya Sera za Ufuatiliaji kwa Serikali zote mbili pamoja na kutenga rasilimali za kutosha kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini.

Aidha amezitaka  Taasisi  hizo kuhakikisha taarifa zinazozalishwa kutokana na kazi za ufuatiliaji na Tathmini zinatumika katika kufanya maamuzi na kuweka mikakati Imara ya kuhabarisha Umma juu ya matokeo ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa kushirikiana na waandishi wa habari ili kufikia malengo ya taasisi na taifa kwa ujumla

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ametowa wito kwa chama cha Wataalamu Afrika ( AFrEA) kuendelea kuvilea vyama vidogo vidogo vilivyomo nchi wanachama pamoja na kuapta fursa za kujifunza na kujiimarisha ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa

Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratib na Bunge Mhe. William Vangimembe Lukuvi amesema katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo nchini kunahitaji uwepo wa taasisi zenye kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ili  kusaidia kulinda matumizi ya  rasilimali fedha zinazotumika katika miradi hio.

Mhe. Lukuvi amesema kuwepo kwa Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza vinaakithi dhamira ya Serikali zote mbili ya kuhakikisha mabadiliko na marekebisho makubwa yanafanyika katika kuimarisha Teknolojia na mifumo ambayo itasaidia kufikia malengo yaliyowekwa na serikali hizo kwa maslahi mapana ya wananchi wa pande zote mbili za muungano.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amesema kufanyika kwa Kongamano la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza hapa Zanzibar litaibua na kupendekeza njia nzuri zaidi za kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini hasa katika masuala ya Utalii na Uwekezaji nchini

Mhe. Sharif amesema kufanyika kwa Ufuatiliaji na Tathmini kunasaidia katika kupima shuhuli za mipango ya maendeleo ya Kimataifa, kitaifa na Kikanda kwa kutathmini ufanisi na uwajibikaji wa Taasisi husika hasa katika kupata taarifa na Takwimu sahihi zenye  matokeo chanya ya mipango hio.

 

ZFDA YAKAMATA BIDHAA ZILIZOPITIWA NA MUDA

 

Na. Fatma Rajab



 

Wakala wa chakula Dawa na vipodozi Zanzibar imefanya Zoezi la kukagua na kushikilia bidhaa mbali mbali  ambazo zimeisha mudawake wamatumizi na ambazo sio sahihi kwa matumizi ya Binaadamu.

Akizungumza na waandushi wa Habari Mkurugenzi Idara ya udhibiti usalama wa chakula Dkt .Khamis  Ali Omar  Ofisini kwake Mombasa wilaya ya Magharibi B amesema katika Zoezi hilo Maalum walishirikiana na jeshi la polisi na uhamiaji  kwa kukagua maeneo mbali mbali ya Biashara ikiwemo  maduka ya vyakula na vipodozi lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata  taratibu zilizowekwa na wakala wa chakula na Dawa  ilikuhakikisha bidhaa hizo zinakuwa salama.

Aidha aliseama  katika zoezi hilo  wamegundua kuwa kuna maduka  mbali mbali ya vipodozi ambayao hayafuati taratibu zilizowekwa hususani katika maduka yaliyopo eneo la Darajani kwa kuuza bidhaa ambazo sio salama kwa matumizi ya bianaadam ambazo wakala wa chakula washazipiga marufuku kutokana na viambata sumu mbali mbali vya bidhaa hizo.

Aidha alisema, katika ukaguzi huo wamefanikiwa kukagua ghala la kampuni ya Cross Boda Treading Company liliopo Tomondo na kugundua takribani ya tani 2.17 za  bidhaa mabli mbali  mchanganyiko  ambazo zimepitwa na Wakati.

Hata hivyo amewataka wafanyabiashara endapo watakua na Biashara  ambazo zimepitwa na wakati wasizitumie  bidhaa hizo na badala yake watoe taarifa  kwa wakala wa chakula na Dawa  ili kuweza kufuata taratibu sahihi za kutekekezwa kwa bidhaa hizo.

Hata hivyo Mkurugenzi Dawa na Vipodozi ametoa wito kwa jamii kuangalia tarehe za mwisho wa bidhaa wanazo zinunua  ili waweze kuepukana  na madhara mbali mbali yanayoweza kujitokeza ambayo yanasbabishwa na wafanyabiashara wa sio waaminifu.

Miongoni mwa Bidhaa zilizokamatwa wakati wa Zeozi hilo katika Ghala la cross Boda ni pamoja ma  Mafuta ya kula lita 970, Bia aina ya savana  lita 340, Maharagwe kilo 210,sweatcorn kilo 567, Maziwa ya Maji lita 78 na Tambi zote hizo ni bidhaa hazifai kwa matumizi ya binaadamu.

 


Vijana watakiwa kujifunza Mafunzo ya Amali Kijikwamua kiuchumi

 Na, Salma   Amour

Kuna umuhimu mkubwa kwa vijana  kujifunza fani zinazotolewa na vyuo vya Mafunzo ya Amali ili Kuweza kujikwamua kimaisha na  kufikia malengo  waliojiwekea.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib  Mhe, Idrisa Kitwana Mustafa.  alipokuwa akuzungumza na wanafunzi wa vyuo vya Amali katika maadhimisho ya  wiki ya vyuo vya amali yaliofanyika  katika chuo cha Green Women Development kwa kushirikiana na chuo cha mafunzo  ya vocatinal training center huko miembeni Zanzibar.

Alisema mafunzo ya amali yana umuhimu mkubwa katika jamii,hivyo ni vyema vijana  kujiunga katika vyuo hivyo ili waweze kupata ujuzi ambao utaweza kuwasaidia katika kujikwamua kimaisha pamoja na kuisaidia Serekali katika suala zima la kuwapatia ajira vijana.

Aidha  alisemakua, inatoa faraja kuona sio viijna   waliopoteza muelekeo katika suala la kielimu  bali hata watu wenye elimu zao wanapata fursa ya kujifunza elimu ya Amali.

Alisema mafunzo ya amali yana umuhimu mkubwa katika jamii,hivyo ni vyema vijana  kujiunga katika vyuo hivyo ili waweze kupata ujuzi ambao utaweza kuwasaidia katika kujikwamua kimaisha pamoja na kuisaidia Serekali katika suala zima la kuwapatia ajira vijana.

Aidha  alisemakua, inatoa faraja kuona sio viijna   waliopoteza muelekeo katika suala la kielimu  bali hata watu wenye elimu zao wanapata fursa ya kujifunza elimu ya Amali.

Aidha Kitwana, ameeleza   vijana wengi walio maliza Degree na walomaliza Darasa la saba wamenufaika kupitia  mafunzo ya amali  hivyo ni vyema  vijana  kuacha  kukata tamaa na badala yake  kujiunga na vyuo vya amali ili waweze  kupata ujuzi ambao  utawawezesha kujiajiri wenyewe.

Hatahivyo alisema serikali ina dhima ya kuweka mnyororo wa thamani kwa lengo la kuwataka wajasiriamali kuuza bidhaa zao ambazo wanazitengeneza na amewataka wafanya biashara kuhifadhi bidhaa zao kwenye vifungashio ili kuepukana na chngamoto mbali mbali ambazo zinazoweza  kujitokeza


Kwa upande wake  Mkurugenzi wa chuo cha Green Women  Development Center. Said Kheir Ame.  amesema anaishukuru wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali kwa kuweka siku Maalum ambayo inawakutanisha viongozi kutoka wizara ya elimu na kutoka vyuoni kwalengo lakujua maendeleo ya  vyuo  hivyo.

Kwa upande wao wanafunzi wanashukuru uwepo wa vyuo vya amali kwani wamekuwa wakijikwamua kimaisha pamoja na kuweza kujiajiri wenyewe na wamewataka vijana wengine ambao wamekata tamaa  kujifunza katika vyuo hivyo ili waweze kupat ujuzi uatkao wawezesha  kujikwamua kimaisha.

Hatahivyo  alisema kua vyuo hvyo  vinatoa mafunzo mbali mblai ikiwemo uandishi wa Habari, mapishi, huduma ya kwanza, uchumi wa buluu,mekup, ufumaji wa mashuka, lugha za kigeni, kupamba  na kupamba steji  mafunzo hayo hutolewa kwa nadharia na vitendo. 


MHE,TABIA ATEMBELEA AMAN COMPLEX

  Na.Fatma Rajab


Waziri wa Habari vijana utamaduni na Michezo Mhe, Tabia Maulid  Mwita amesema amaeridishwa na  ujenzi wa sehemu ya pili unaoendelea katika viwanja  vya new amani complex

Ameyasema hayo wakati alipokua katika ziara ya kukagua  sehemu ya pili  ya mradi wa ujenzi katika viwanja vya new amani complex wilaya ya mjini unguja.

Alisema kulikua na hatua ya ujenzi wa mradi huo ambao ulikua haujakamilika hivyo alisema lengo la kufanya ziara hiyo ni kukagua majengo mbali mbali ambayo yalikua hayajakamilika na amekagua hoteli, migahawa, ukumbi mkubwa wa mikutano wa kimataifa pamoja na maholi ya kuchezea michezo ya ndani.

Aidha alisema "mradi huo umefikia 99% kwa mujibu wa mshauri elekezi na hatua iliyofikia ni hatua ya kukerebisha baadhi ya makosa na wanategemea mnamo tarehe 9 mwezi huu wa 9 mradi huo utakabidhiwa  rasmini kutoka kwa mkandarasi na kwenda kwa wizara na hatua zitakazofuata ni hatua za kiserikali za kufungua na kuzinduwa miradi hiyo"

Pia alisema katika ukaguzi huo aliona makosa katika mapaa ya juu ya mduka kua ni dhaifu na hayana ubora na ametoa maelekzo katika kampuni ya kubadilisha mabati hayo kwa kuweka mabati yaliyokuwa imara ndani ya kipindi cha muda mfupi usiozidi wiki moja ili waweze kuendelea na utaratibu wa kukodisha maduka kwa lengo la kuweza kupata kipato katika wizara pamoja na serikali kwa ujumla

Sambamba na hayo alitoa wito kwa kusema"miradi hiyo imeshakamilika lakini kuna miradi ambayo inajumuisha wafanyabiashara ikiwemo miradi ya maduka hivyo tunawakaribisha watu katika wizara yetu kuandika barua na kufanya maombi ya kukodi maduka hayo

Hata hivyo alisema" sio kila biashara  itatakiwa kufanywa katika maduka hayo isipokuwa wizara itafanya utaratibu maalum wa kujua ni biashara  gani ambayo  itatakiwa kufanywa katika maduka hayo na kumewekwa kipaumbele zaidi kwa wafanyabiashara wanaouza vifaa vya michezo na biashara nyengine ambazo zitaendana na sehemu hiyo na wamemuomba mkandarasi ndani ya mda mfupi wa wiki mbili kukamilisha marekebisho yote ambayo amepatiwa  awe ameyakamilisha na aweze kutukabidhi mradi huu ili utaratibu mwengine wa matumizi uweze kuendelea"

 

WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA VYEMA FURSA ZA MASOMO YA SAYANSI NCHINI.

 

Na Fatma Rajabu 


Mkurugenzi dhamana wa Taasisi ya Teknolojia ya india madrasa kampasi ya zanzibar (IITMZ) Professa PREETI  AGHALAYAM  amewataka  wanafunzi wanaosomea masoma ya sayansi kuzitumia vyema fursa za kimasomo zinazotolewa na taasisi ya (IITMZ).

Ameeleza hayo katika ziara iliyofanywa na wanafunzi wa skuli ya sekondari hasnuu makame wakati   waliotembelea  kampasi ya IIT madrasa  kwa lengo la kujigunza.

Alisema kuwa taasisi ya IIT madrasa  imefungua fursa mbali mbali za maendekeo ya kielimu baina ya Tanzania, india na mataifa mengine miongoni mwa fursa hizo ni : fursa za mashirikiano ya   kiutendaji kwa taasisi yenye lengo la kukuza utendaji wa kazi kwa taasisi jambo ambalo litaleta maendeleo mazuri  na ukuaji  taasisi hizo.

Aidha alisema kuwa IIT Madrasa inamatarajio makubwa kwa wahitimu wa kudato cha sita ambao wanasoma masomo ya sayansi katika kujiunga na taasisi hiyo ikizingatiwa fani zinazotolewa zina lengo la kurahisisha utoaji wa huduma za kijamii kwa kutumia elimu ya kisayansi na teknolojia ya kisasa ili kuwenda sambmba na mahitaji ya ulimwengu wa kisasa

Kwa upande wake Mkuu wa Taaluma kutoka Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame Mwalimu Jecha Simai alitoa shukrani kwa walimu wa IIT madrasa kwa kuendelea kutoa utoaji wa fursa  za kimasomo kwa vitendo pamoja na kuendesha mazoezi ya kuwasajihisha wanafunzi kuendelea kuyapenda masomo ya sayansi.

Nao wanafunzi wametoa maoni yao kwa kusema wamefurahishwa kuona miundombinu tofauti ya kiteknolojia iliyopo katika kampasi ya IIT Madrasa  inayotumika kutolea taaluma na amewataka walimu  kuendeleza ziara  za kimasoma kwa wanafunzi ikiwa ni njia moja wapo ya kujenga uhalisia wa masomo yao.

Ziara hiyo ya siku moja ya wanafunzi wa skuli ya Sekondari Hasnuu Makame katika kampasi ya IIT madrasa imehusisha jumla ya wanafunzi sitini na nane wa kidato cha sita wanaosomea masomo ya sayansi na walimu saba.

Mikakati Imara inahitajika kuleta Mabadiliko Katika Jamii

 

Na Fatma Rajab.



Wahasibu wanawake Tanzania wametakiwa kuweka mikakati Imara na thabiti ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla ili kuweza kutanua wigo mpana wa kuhamasisha usawa na haki kwa wanawake na wasichana Tanzania.

Hayo yamesemwa na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. HEMED SULEIMAN ABDULLA wakati akifungua Kongamano la Saba(7) la Uongozi la Wanawake Wahasibu Tanzania kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hotel  ya  Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Amesema wahasibu wanawake wana fursa ya kujenga mtandao Imara wa kusaidiana na kuhamasishana kufikia maendeleo waaliokusudia hasa  katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Rais Dkt. Samia amesema Serikali itaendelea kuwa washirika wa kimkakati na kusimama pamoja na TAWCA katika kuboresha mazingira ya kazi, kuwekeza katika elimu, fursa sawa za maendeleo pamoja na  kuondoa vikwazo dhidi ya wanawake kwa kuwaandaa kuwa viongozi wa kesho wanaotokana na wanawake wahasibu nchini.

Aidha Dkt Samia amesema kuwa TAWCA imekuwa mstari wa Mbele katika kuwainua wajasiriamali kwa kuwapa taaluma za kifedha na stadi za maisha ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea katika biashara zao.

Dkt Samia amekipongeza chama cha wahasibu wanawake Tanzania kwa shuhuli mbali mbali wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa wanawake, kuwasaidia wahasibu wachanga kuweza kufanya vizuri katika fani zao kwa kuwakumbusha kuzingatia maadili ya kazi zao

Sambamba na Hayo ametoa wito kwa wadau mbali mbali kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia upatikanaji wa kundi bora la wanawake lenye kujitegemea katika kuboresha na kuinua uchumi katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Nae Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Juma Makungu Juma amesema Serikali inatambua mchango wa wanawake wahasibu nchini katika kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa hivyo itaendelea kufanya kazi kwa karibu na TAWCA ili kufika malengo ya kuanzishwa kwa Chama hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la TAWCA, CPA Neema Kiure amesema lengo la kongamano hilo ni kuwajengea uwezo na kupeana taaluma na ujuzi kwa wahasibu wanawake ili kuchochea mabadiliko ya kiutendaji na kimaendeleo katika kada ya uhasibu nchini.




Amesema TAWCA imekuwa ikitoa elimu kwa wajasiriamali wanawake juu ya kutunza kumbukumbu za biashara na namna ya matumizi mazuri ya mikopo wanayopatiwa ili waweze kupata matokeo yenye tija na faida zaidi.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa wahasibu na Wakaguzi wa hesabu Tanzania(NBAA) CPA Pius Maneno amesema taaluma ya uhasibu inakuwa kwa kasi Tanzania ambapo hadi kufikia mwaka 2024 wahasibu wanawake waliosajiliwa wamefikia asilimia 34% na ambao wanasaidia kufikisha elimu ya utunzaji wa fedha kwa wafanyabiashara na wajasiri amali nchini.

CPA Maneno amesema kazi kubwa inayofanywa na TAWCA ni kudhibiti na kusimamia taaluma ya uhasibu kwa kuwapatia ujuzi na nyenzo wahasibu wanawake za kuweza kuwafikia wanawake na wasichana nchini kuwapa elimu ya biashara na ujasiriamali ili  kujikwamua kimaisha.

 


Serikali kuchukua Juhudi kukabiliana na Madawa ya Kulevya.

 

Na, Mwandishi Wetu.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema Tanzania  imekuwa ikuchukua jitihada mbali mbali katika kukabiliana na tatizo la dawa  za kulevya kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria za dawa za kulevya hapa nchini

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Kamisheni ya Kupambana na dawa za kulevya kwa nchi zilizo Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni  Zanzibar.

Amesema Tanzania imedhamiria kutekeleza Sera na mikakati madhubuti ya udhibiti wa dawa za kulevya kwa kudhibiti utengenezaji, uingizwaji, usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini ili kupunguza athari zitokanazo na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo vitendo vya kihalifu, biashara haramu, utakatishaji wa fedha na ugaidi.

Rais Dkt Mwinyi amesema kuwa Tanzania imekuwa ikiimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa katika kukabiliana na dawa za kulevya kwa kuzijengea uwezo Taasisi zinazoshiriki katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ili kuweza kufikia lengo la kutokomeza matumizi ya madawa hayo hapa nchini.

Aidha Dkt Mwinyi amesema Tanzania   inatambua umuhimu wa kuwa na sera madhubuti yenye kutoa miongozo ya kisheria, tiba, elimu yenye kuainisha miongozo jumuishi na ushirikiano kwenye ngazi zote ikiwemo kujikita katika kinga na kutambua mapema viashiria vya biashara na matumizi ya dawa za kulevya ili kuzuia  madhara yanayoweza kujitokeza

Sambamba na hayo Rais Dkt. Mwinyi amevipongeza vyombo vya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kukabiliana na kupambana na dawa za kulevya kwa lengo la kuhakikisha Tanzania na Watanzania wanakuwa salama kutokana janga la dawa za kulevya linaloathiri Afya na Ustawi wa Wananchi hasa vijana.

Nae Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhandisi HAMAD YUSSUF MASAUNI amesema Jitihada mbali mbali zimekuwa zikichukuliwa na Serikali zote Mbili kwa kusimamia kikamilifu sheria za kudhibiti dawa za kulevya kwa kudhibiti usambazaji, Uuzaji na utumiaji wa dawa.

Amesema Serikali kupitia Mamlaka husika za kupambana na dawa za kulevya zimekuwa zikitoa  elimu kwa wananchi na waathirika wa dawa hizo kupitia vyombo vya habari pamoja na kuwatembelea katika vituo vya  vya tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya.

Mhe. MASAUNI amefahamisha kuwa vyombo vya Ulinzi na Usalama vimekuwa vikipambana kikamilifu kuhakikisha vinadhibiti uingizwaji wa dawa ya kulevya kwa kuimarisha ulinzi hasa katika maeneo ya mipakani ambayo hutumika kwa kuingizia dawa hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Kupambana na dawa za kulevya kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika Mhe. KGALEMA MONTLANTHE amesema dawa za kulevya kwa sasa ni janga hatari duniani kote hivyo Sera na Mikakati madhubuti inahitajika ili  kutokomeza kabisa dawa hizo  hasa kwa nchi wanachama.

Amesema Tume ya kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na wadau mbali mbali  wanaendelea  kutafuta mbinu mpya na Sera jumuishi za kukabiliana na dawa za kulevya kwa lengo la kuwadhibiti wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo

Amesema Mkutano huo wa siku mbili utatoa fursa kwa washiriki  kubadilishana Ujuzi na mbinu bali mbali za kufukia lengo la kudhibiti na kutokomeza dawa za kulevya kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.


Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar

Na, Mwandisho.   Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowa...