NA, Fatma Rajab
Waziri wa viwanda na Biashara
Tanzania Mhe. Suleiman Said Jafo amesema maonesho ya 11 ya biashara ni jukwaa
muhumu la ukuzaji wa sekta ya biashara na uwekezaji nchini.
Akifungua maonesho ya 11 ya biashara
Zanzibar huko Nyamazi alisema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata
taarifa mbali mbali za kibiashara hali inayopelekea ukuaji wa biashara na
uchumi na uwekezaji nchini.
Katika kuboresha maonesho hayo Waziri
Jafo aliziomba Wizara husika kuhakikisha inajenga majengo ya kudumu katika
maonesho hayo ili kuweka mazingira mazuri ya maonesho hayo.
Katibu mkuu wizara ya maendeleo ya
viwanda na biashara Zanzibar bi Fatuma Mbarouk alisema maonesho hayo tangu
yalipoanzishwa mwaka 2014 yamekuwa
chachu ya ukuaji wa biashara nchini
kutokana na kuengezeka kwa wafanya biashara mwaka Hadi mwaka
Mapema Mwenyekiti wa jumuiya ya
wafanya biashara Zanzibar Ali Suleimani Amour aliiomba serikali kuhakikisha kua
kampuni binafsi zinapewa fursa za kuandaa maonesho makubwa kama hayo ili kutoa
fursa ya ushindani mkubwa wa kibiashara nchini.
Maonesho hayo ambayo yanabeba kauli mbiu ya biashara mtandao kwa maendeleo ya uchumi na uwekezaji yameshirikisha wafanya biashara kutoka sekta mbali mbali za kibiashara wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania
No comments:
Post a Comment