Na,Fatam Rajab
Jamii
imetakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa katika kuwalea watoto katika maadili mema yenye kupwekesha Mwenyezi
Mungu.
Hayo
yameelezwa nakatibu wa kamati ya maadili kupitia baraza na Taasisi za kiislamu
Zanzibar Abdalla Mnubi Abas ambae ni katibu wa kamati ya maadili kupitia
Jumuiya ya maimamu Zanzibar wakati alipokuwa katika muhadhara wa kujadili suala
zima la maadili kwa watoto katika kijiji cha banda kuu Nungwi Zanzibar.
Amesema
vyuo vya madrasa vina umuhimu mkubwa
katika jamii na ni njia moja ya watoto
kukuwa katika maadili mema na sehemu
pekee ya kurudisha maadili katika jamii ni vyuo vya Qurani ambayo hufundisha tabia njema na kuacha tabia mbaya zisizokuwa
na maadili
Aidha
amesema"kutokana na uvamizi uiliopo katika kijiji cha Nungwi kuwepo kwa
mahoteli na wageni mbali mbali ambao wanatoka ndani ya nchi na nje ya nchi kutofuata
maadili na kuvaa vivazi ambavyo havifai.
Aidha,amewataka
wazazi na walezi kuiga malezi ambayo waliolelewa na wazee wa zamani na kuishi
kirafiki na watoto wao ili kugundua changamoto wanazo kumbana nazo.
Kwa
upande wake sheha wa shehia ya bandaa kuu Nungwi Haji Khamis Haji amesma tatizo la maadili limekuwa kubwa
katika jamii na linatokana na changamoto mbali mbali ikiwemo mazizngira, wigo, na
uingiaji wa wageni kiholela.
Amesema mikakati mabli mbali ambayo
imechukuliwa katika kijiji hicho ikiwemo ya kiwekwa mihadhra yenye kuelimisha
watu katika suala zima la maadili, pia amesisitiza wazazi na walezi kukaa
karibu na watoto wao na kuwap elimu kuhisiana na masula ya kumcha Allah ili waweze
kuepukana na vitendo viovu.
Akitoa
wito kwa wageni Ndg Haji Khamis Haji amesema "wageni wanatakiwa kungalia
jamii inaishi vipi ili kuepusha upotevu wa maadaili endapo watafika katika
jamii na wanatakiwa kuzingatia sharia za sehemu husika.
Hata
hivyo wazazi na walezi wa kijiji hicho wamaitaka jumuiya
ya maimu kuwasaidia katika malezi na kukza maadili ya jamii ili kuwa na
kazazi chema chenye kufuata maadili mema .
No comments:
Post a Comment