NA FATMA RAJAB
Zanzibar, imejikita kwenye
kilimo cha biashara kama mwani, viungo na Ujasiriamali ambao umewajumuisha
zaidi wanawake wanao jishughulisha na
utengenezaji wa mafuta ya mimea, sabuni, utengenezaji vitambaa na sanaa za
mikono
Katibu Mkuu Wizara ya
Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma Mabrouk Khamis ameyasema hayo katika
mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael A. Battle akiambatana
na Maafisa biashara kutoka Ubalozi wa Marekani kwa lengo la kujitambulisha na
kufanya mazungumzo ya kuimarisha Mashirikiano ya Kibiashara kati ya Marekani na
Tanzania kwa upande wa Zanzibar.
Mazungumzo hayo,
yamefanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Maruhubi, ambapo
Bi Fatma amefafanua pande zote mbili zimekubaliana kuwa na mpango wa kuandaa
eneo la kibiashara ambalo litaleta tija.
Aidha mazungumzo hayo
yamelenga kuimarisha uvuvi kutokana na
Zanzibar kuwa na eneo kubwa la
Uvuvi wa baharini (Deep sea fishing)
linalohitaji kuimarishwa zaidi.
Kwa upande wa Ubalozi wa
Marekeani wamesema kuwa wapo tayari kushirikiana na Zanzibar kutoa Misaada ya kitaalamu pale inapohitajika
ili kuisaidia Zanzibar kufikia katika soko la AGOA na masoko mengine kutokana
na Zanzibar inatambulika ulimwenguni kwa biashara ya Utalii.
mazungumzo hayo ya siku
moja yameangalia maeneo muhimu ya kibishara ambayo ni pamoja na uchumi wa
kidijitali (digital economy), Mabadiliko ya Sheria katika Biashara, upatikanaji
wa Masoko na kuanzishwa misafara ya Kibiashara.
No comments:
Post a Comment