ZSTC yaridhiishwa na Chuo cha Mafunzo Katika Uimarishaji wa Zao la Karafuu

 


Na. Mwandishi Wetu.




Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Nd. Soud Said Ali amesema Shirika la Biashara Zanzibar limeridhishwa na kazi ya uimarishaji wa zao la karafuu inayofanywa na Chuo cha Mafunzo Zanzibar.

 Mkurugenzi Soud amesema hayo katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya uatikaji miche ya mikarafuu Chuo cha Mafunzo Langoni.

“Shirika linaridhishwa na kazi nzuri mnayofanya Chuo cha Mafunzo ya kuimarisha zao la karafuu na Shirika litaendelea kuunga mkono ili kuhakikisha zao hili linarudi katika asili yake”. Alifahamisha Mkurugenzi Soud,

“Chuo cha Mafunzo mna maeneo mazuri kwa upandaji wa mikarafuu na nguvu kazi ya kutosha hivyo kwa pamoja tunaweza kufanikiwa katika jitihada hizi za kuimarisha zao la karafuu na kuongeza uzalishaji”. Alisisitiza Mkurugenzi Soud.

Aidha juhudi hizo za umiarishaji wa zao la karafuu zitaendelea kwa utoaji wa vifaa vya uatikaji wa miche ya mikarafuu kwa vitalu vya wakulima binafsi na Wizara ya Kilimo


Kwa upende wake Kamishna Msaidizi Chuo Cha Mafunzo Zoni ya Mashamba ACP Amour Naimu Khamis. amesema kuwa Chuo cha Mafunzo kinashukuru na kuthamini mashirikiano baina yake na Shirika la ZSTC katika uimarishaji wa zao la karafuu.

Alisema kuwa, Chuo cha Mafunzo kitatumia vifaa na elimu wanayoipata Kutoka ZSTC katika kupanda na kuihudumia mikarafuu kwa maslahi ya Chuo, ZSTC na Serikali.

ZSTC na Chuo cha Mafunzo Zanzibar wameingia katika  makubaliano na mashirikiano ya kuimarisha zao la karafuu kwa kupanda mikarafuu katika mashamba ya chuo cha Mafunzo, uanzishwaji wa kitalu cha miche ya mikarafuu, uchimbaji  wa visima na miundombinu ya umwagiliaji.

Katika hafla hiyo Mkurugenzi Soud alikabidhi vifaa mbali mbali kwa ajili ya uoteshaji miche ya mikarafuu ambayo itapandwa katika mashamba ya Chuo cha Mafunzo Langoni na Kinumoshi.

 

 


No comments:

Post a Comment

ZSTC yaridhiishwa na Chuo cha Mafunzo Katika Uimarishaji wa Zao la Karafuu

  Na. Mwandishi Wetu. Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Nd. Soud Said Ali amesema Shirika la Biashara Z...