Na.Fatma Rajab
Waziri wa Habari vijana
utamaduni na Michezo Mhe, Tabia Maulid
Mwita amesema amaeridishwa na
ujenzi wa sehemu ya pili unaoendelea katika viwanja vya new amani complex
Ameyasema hayo wakati
alipokua katika ziara ya kukagua sehemu
ya pili ya mradi wa ujenzi katika
viwanja vya new amani complex wilaya ya mjini unguja.
Alisema kulikua na hatua ya
ujenzi wa mradi huo ambao ulikua haujakamilika hivyo alisema lengo la kufanya
ziara hiyo ni kukagua majengo mbali mbali ambayo yalikua hayajakamilika na
amekagua hoteli, migahawa, ukumbi mkubwa wa mikutano wa kimataifa pamoja na
maholi ya kuchezea michezo ya ndani.
Aidha alisema "mradi
huo umefikia 99% kwa mujibu wa mshauri elekezi na hatua iliyofikia ni hatua ya
kukerebisha baadhi ya makosa na wanategemea mnamo tarehe 9 mwezi huu wa 9 mradi
huo utakabidhiwa rasmini kutoka kwa
mkandarasi na kwenda kwa wizara na hatua zitakazofuata ni hatua za kiserikali
za kufungua na kuzinduwa miradi hiyo"
Pia alisema katika ukaguzi
huo aliona makosa katika mapaa ya juu ya mduka kua ni dhaifu na hayana ubora na
ametoa maelekzo katika kampuni ya kubadilisha mabati hayo kwa kuweka mabati
yaliyokuwa imara ndani ya kipindi cha muda mfupi usiozidi wiki moja ili waweze
kuendelea na utaratibu wa kukodisha maduka kwa lengo la kuweza kupata kipato
katika wizara pamoja na serikali kwa ujumla
Sambamba na hayo alitoa
wito kwa kusema"miradi hiyo imeshakamilika lakini kuna miradi ambayo
inajumuisha wafanyabiashara ikiwemo miradi ya maduka hivyo tunawakaribisha watu
katika wizara yetu kuandika barua na kufanya maombi ya kukodi maduka hayo
Hata hivyo alisema"
sio kila biashara itatakiwa kufanywa
katika maduka hayo isipokuwa wizara itafanya utaratibu maalum wa kujua ni
biashara gani ambayo itatakiwa kufanywa katika maduka hayo na
kumewekwa kipaumbele zaidi kwa wafanyabiashara wanaouza vifaa vya michezo na
biashara nyengine ambazo zitaendana na sehemu hiyo na wamemuomba mkandarasi
ndani ya mda mfupi wa wiki mbili kukamilisha marekebisho yote ambayo
amepatiwa awe ameyakamilisha na aweze
kutukabidhi mradi huu ili utaratibu mwengine wa matumizi uweze kuendelea"
No comments:
Post a Comment