Na Fatma Rajabu
Mkurugenzi dhamana wa Taasisi
ya Teknolojia ya india madrasa kampasi ya zanzibar (IITMZ) Professa PREETI AGHALAYAM
amewataka wanafunzi wanaosomea
masoma ya sayansi kuzitumia vyema fursa za kimasomo zinazotolewa na taasisi ya
(IITMZ).
Ameeleza hayo katika ziara
iliyofanywa na wanafunzi wa skuli ya sekondari hasnuu makame wakati waliotembelea kampasi ya IIT madrasa kwa lengo la kujigunza.
Alisema kuwa taasisi ya IIT
madrasa imefungua fursa mbali mbali za
maendekeo ya kielimu baina ya Tanzania, india na mataifa mengine miongoni mwa
fursa hizo ni : fursa za mashirikiano ya
kiutendaji kwa taasisi yenye lengo la kukuza utendaji wa kazi kwa
taasisi jambo ambalo litaleta maendeleo mazuri
na ukuaji taasisi hizo.
Aidha alisema kuwa IIT
Madrasa inamatarajio makubwa kwa wahitimu wa kudato cha sita ambao wanasoma
masomo ya sayansi katika kujiunga na taasisi hiyo ikizingatiwa fani
zinazotolewa zina lengo la kurahisisha utoaji wa huduma za kijamii kwa kutumia
elimu ya kisayansi na teknolojia ya kisasa ili kuwenda sambmba na mahitaji ya
ulimwengu wa kisasa
Kwa upande wake Mkuu wa
Taaluma kutoka Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame Mwalimu Jecha Simai alitoa
shukrani kwa walimu wa IIT madrasa kwa kuendelea kutoa utoaji wa fursa za kimasomo kwa vitendo pamoja na kuendesha mazoezi
ya kuwasajihisha wanafunzi kuendelea kuyapenda masomo ya sayansi.
Nao wanafunzi wametoa maoni
yao kwa kusema wamefurahishwa kuona miundombinu tofauti ya kiteknolojia iliyopo
katika kampasi ya IIT Madrasa
inayotumika kutolea taaluma na amewataka walimu kuendeleza ziara za kimasoma kwa wanafunzi ikiwa ni njia moja
wapo ya kujenga uhalisia wa masomo yao.
Ziara hiyo ya siku moja ya
wanafunzi wa skuli ya Sekondari Hasnuu Makame katika kampasi ya IIT madrasa
imehusisha jumla ya wanafunzi sitini na nane wa kidato cha sita wanaosomea
masomo ya sayansi na walimu saba.
No comments:
Post a Comment