Na, Fatma Rajab
Wadau wa michezo kwa maendeleo Zanzibar ikiwemo Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania, (TAMWA ZNZ), Chama Cha wanasheria wanawake ZAFELA, Ktuo cha Mijadala kwa Vijana (CYD) pamoja na Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ) wameandaa shughuli mbali mbali za Michezo kwa maendeleo yenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika michezo na kujikinga na udhalilishaji wa kijinsia kijinsia katika
Hayo yameelezwa na
Afisa programu kutoka TAMWA (ZNZ) Khairat
Haji Ali wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika ukumbi wa
mkutano wa viwanja vya mau Zanzibar.
Amesema maadhimisho hayo yana lengo la kuimarisha watoto wa kike kushiriki katika michezo pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambayo kwa asilimia kubwa vinawakumba watoto wa kike.katika michezo
Aidha amesema,
kuelekea maadhimisho hayo wameandaa ziara ya kutembelea Skuli mbali mbali na
kuendesha shughuli za michezo kwa maendeleo na kuwafundisha wanafunzi jinsi ya
kujikinga na vitendo vya udhalilishaji pamoja na kuwaelimisha wanafunzi wa kike
juu ya suala zima la wanawake na uongozi.
Hata hivyo amesema kuwa maadhimisho hayo
yatashirikisha wanafunzi kutoka Skuli za Unguja kutoka wilaya ya Kaskazini A,
wilaya ya mjini, Wilaya ya Kati pamoja na wilaya ya Magharibi A ‘’madhimisho hayo yataanza na shamra shamra za michezo ya
aina tofauti ikiwemo mchezo wa Mpira wa
Pete (Netball), na michezo mengine itakayohusisha timu za watoto wa kike kutoka
Skuli ya Tumbatu, jongowe, Mkokotoni, Mtowa pwani, Kianga, Mtoni, Kiembesamaki
B na Uroa’’. Amesema Khairat.
Kwa upande wake Rahma
Ali Juma kutoka kituo Cha Mijadala kwa vijana (CYD) amesema katika michezo hiyo
itahusisha pia watoto wenye Ulemavu kwani nao wana haki ya kushiriki katika michezo kama watoto wengine .
Kilele cha madhimisho
hayo kina tarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya Tarehe 12 Oktoba,2024 kwa
kuanzia na mechi ya finali ya mpira wa Pete (netball) pamoja na kuoneshwa picha
zilizochorwa na wanafunzi.Kauli mbiu ya
maadhimisho hayo ni "muwezeshe mtoto wa kike apaze sauti yake"
No comments:
Post a Comment