Na, Asia Hakim.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema Taaluma ua Ukaguzi wa ndani ni
msingi wa uadilifu na mafanikio kwa Taasisi za Umma na binafsi zinashuhulika na
Taaluma hio.
Ameyasema hayo kwa niaba
ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein
Ali Mwinyi katika ufunguzi wa Mkutano
wa Kumi na Saba (17) wa Wakaguzi wa
ndani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
ya Kimataifa jijini Arusha.
Amesema kutokana na jukumu la ukaguzi wa ndani kuwa ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa ni wajibu wa
wakaguzi wa ndani kukusanya nguvu za pamoja katika kujenga mustakbali wenye mafanikio zaidi,
usawa endelevu na utawala bora nchini.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa wakaguzi wa ndani ni mabingwa wa utawala bora, walinzi wa uwadilifu, na ni watu wenye viwango vikubwa vya maadili hivyo huhakikisha kuwa taasisi zao zinafanya kazi kwa viwango vikubwa, uwajibikaji, uwazi na uaminifu kwa wananchi, wafanyabiashara na washirika wa Kimataifa ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo.
Mhe. Hemed amesema Serikali
inatambua umuhimu mkubwa wa kudumisha uhuru na usawa wa wakaguzi wa ndani hivyo
Serikali iko imara katika kuzingatia kanuni za ukaguzi wa ndani ili kuhakikisha
wanafanya kazi zao bila ya ushawishi usiofaa na kutokuingiliwa katika majukumu
yao ya kila siku.
Aidha, Makamu wa Pili wa
Rais amewahakikishia wakaguzi wa ndani kuwa Serikali inatambua na kuunga mkono
kikamilifu jukumu muhimu la ukaguzi wa ndani hivyo itahakikisha inaimarisha
mfumo unaowezesha kazi zao, kuongeza uwezo wa ukaguzi wa kitaaluma na kukuza
utamaduni wa uwajibikaji katika Taasisi zote.
Sambamba na hayo Mhe.Hemed
ametoa wito kwa wakaguzi wa ndani kuutumia Mkutano huo katika kujadiliana na
kubadilishana mawazo chanya yatakayoleta uvumbuzi na maarifa zaidi katika
kuendeleza Taaluma hio kwa mustakabali mwema wa maendeleo ya Taasisi zetu na
Taifa kwa ujumla.
Nae Rais wa Taasisi ya
Ukaguzi wa Ndani Tanzania ( I I A )Dkt. ZALIA NJEZA amesema lengo la kuwepo kwa
Mkutano wa wakaguzi wa ndani ni kujadiliana njia mbali mbali zitakazo wawezesha
kufanya kazi zao kwa uadilifu na
uwajibikaji na kuisaidia Serikali
kufanya kazi za ukaguzi kwa ufanisi na
kwa viwango vya hali ya juu.
Dkt ZALIA amesema Taasisi
ya Ukaguzi wa Ndani Tanzania imekuwa na jukumu la kuhakikisha wanachama wake
wanaendelezwa kielimu, kutanua wigo wa mtandao wa wanataaluma ya ukaguzi ndani
na nje ya nchi pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili
na uamifu ili kuisaidia Serikali katika uwajibikaji hasa wa udhibiti wa matumizi ya rasilimali fedha.
Amesema Taasisi ya Wakaguzi
wa ndani itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali zote mbili pamoja na
wadau wao ili kurahisisha ufanyaji kazi kupitia taaluma hio kwa kuwa na Wakaguzi wa ndani wenye
taaluma, ujuzi na viwango vye ubora
katika ukaguzi wa ndani.
Kwa upande wake Mkaguzi
Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CPA BENJAMIN MASHAURI MAGAI
amesema Ukaguzi wa ndani ni eneo muhimu endapo litaimarishwa na litaisaidia
Serikali na Taasisi binafsi kuangalia rasilimali za nchi, udhibiti wa mifumo ya
ndani , viashiria vya upotevu wa rasilimali na kusimamia ulinzi katika matumizi
ya rasilimali kwa Taasisi zote nchini.
CPA .MASHAURI amesema wakaguzi wa ndani nchini wamekuwa
wakikabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa na rasilimali fedha hada pale wanapolazimika
kufanya kazi nje ya maeneo yao ya kazi
jambo ambali linawapa wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kwa
uweledi na ufanisi zaidi hivyo wameziomba serikali kuweza kuwatatulia
changamoto zinazowakabili ili kuwarahisishia ufanyaji wa kazi zao.
Akitoa salamu za Mkoa wa
Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo CRISTIAN PAUL MAKONDA, Mkuu wa Wilaya ya
Munduli FESTO SHEM KITEANGWA amesema Serikali imathamini jukumu muhimu
linalifanywa na wakaguzi wa ndani katika kuisaidi Serikali kupiga hatua za
kimaendeleo hasa katika udhibiti wa rasilimali katika Taasisi za umma na
Taasisi binafsi nchini.
KISANGA amesema Mkutano huo
ukawe chachu na kutoa fursa ya kusaidiana na kuendelezana kitaaluma,
kubadilishana uzoefu pamoja na kuweka mikakati imara ya kufikia malengo ya Taasisi
hiyo na Taifa kwa ujumla.
Mapema Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amekagua mabanda ya maonesho na
kujionea kazi mbali mbali zinazofanywa na wakaguzi wa ndani walioshiriki katika
ufunguzi wa Mkutano wa Kumi na Saba(17) wa Taasisi ya Wakaguzi wa ndani
Tanzania kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi yaliyopo
nje ya Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa
jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment