Na, Salma Amour
Kuna
umuhimu mkubwa kwa vijana kujifunza fani
zinazotolewa na vyuo vya Mafunzo ya Amali ili Kuweza kujikwamua kimaisha
na kufikia malengo waliojiwekea.
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe, Idrisa Kitwana Mustafa. alipokuwa akuzungumza na wanafunzi wa vyuo
vya Amali katika maadhimisho ya wiki ya
vyuo vya amali yaliofanyika katika chuo
cha Green Women Development kwa kushirikiana na chuo cha mafunzo ya vocatinal training center huko miembeni Zanzibar.
Alisema
mafunzo ya amali yana umuhimu mkubwa katika jamii,hivyo ni vyema vijana kujiunga katika vyuo hivyo ili waweze kupata
ujuzi ambao utaweza kuwasaidia katika kujikwamua kimaisha pamoja na kuisaidia Serekali
katika suala zima la kuwapatia ajira vijana.
Aidha alisemakua, inatoa faraja kuona sio viijna waliopoteza muelekeo katika suala la kielimu bali hata watu wenye elimu zao wanapata fursa ya kujifunza elimu ya Amali.
Alisema
mafunzo ya amali yana umuhimu mkubwa katika jamii,hivyo ni vyema vijana kujiunga katika vyuo hivyo ili waweze kupata
ujuzi ambao utaweza kuwasaidia katika kujikwamua kimaisha pamoja na kuisaidia Serekali
katika suala zima la kuwapatia ajira vijana.
Aidha alisemakua, inatoa faraja kuona sio
viijna waliopoteza muelekeo katika
suala la kielimu bali hata watu wenye
elimu zao wanapata fursa ya kujifunza elimu ya Amali.
Aidha
Kitwana, ameeleza vijana wengi walio maliza Degree na walomaliza
Darasa la saba wamenufaika kupitia
mafunzo ya amali hivyo ni vyema vijana
kuacha kukata tamaa na badala
yake kujiunga na vyuo vya amali ili
waweze kupata ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri wenyewe.
Hatahivyo
alisema serikali ina dhima ya kuweka mnyororo wa thamani kwa lengo la kuwataka
wajasiriamali kuuza bidhaa zao ambazo wanazitengeneza na amewataka wafanya
biashara kuhifadhi bidhaa zao kwenye vifungashio ili kuepukana na chngamoto
mbali mbali ambazo zinazoweza kujitokeza
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa chuo cha Green
Women Development Center. Said Kheir Ame.
amesema anaishukuru wizara ya elimu na
Mafunzo ya Amali kwa kuweka siku Maalum ambayo inawakutanisha viongozi kutoka
wizara ya elimu na kutoka vyuoni kwalengo lakujua maendeleo ya vyuo hivyo.
Kwa
upande wao wanafunzi wanashukuru uwepo wa vyuo vya amali kwani wamekuwa
wakijikwamua kimaisha pamoja na kuweza kujiajiri wenyewe na wamewataka vijana
wengine ambao wamekata tamaa kujifunza
katika vyuo hivyo ili waweze kupat ujuzi uatkao wawezesha kujikwamua kimaisha.
Hatahivyo alisema kua vyuo hvyo vinatoa mafunzo mbali mblai ikiwemo uandishi
wa Habari, mapishi, huduma ya kwanza, uchumi wa buluu,mekup, ufumaji wa
mashuka, lugha za kigeni, kupamba na
kupamba steji mafunzo hayo hutolewa kwa
nadharia na vitendo.
Ni nxuri Sanna kuliko kukaa kusubiri ajira.
ReplyDelete