Na. Fatma Rajab
Wakala wa chakula Dawa na vipodozi Zanzibar imefanya Zoezi la kukagua na kushikilia bidhaa mbali mbali ambazo zimeisha mudawake wamatumizi na ambazo sio sahihi kwa matumizi ya Binaadamu.
Akizungumza na waandushi wa Habari Mkurugenzi Idara ya udhibiti usalama wa chakula Dkt .Khamis Ali Omar Ofisini kwake Mombasa wilaya ya Magharibi B amesema katika Zoezi hilo Maalum walishirikiana na jeshi la polisi na uhamiaji kwa kukagua maeneo mbali mbali ya Biashara ikiwemo maduka ya vyakula na vipodozi lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata taratibu zilizowekwa na wakala wa chakula na Dawa ilikuhakikisha bidhaa hizo zinakuwa salama.
Aidha
aliseama katika zoezi hilo wamegundua kuwa kuna maduka mbali mbali ya vipodozi ambayao hayafuati
taratibu zilizowekwa hususani katika maduka yaliyopo eneo la Darajani kwa kuuza
bidhaa ambazo sio salama kwa matumizi ya bianaadam ambazo wakala wa chakula
washazipiga marufuku kutokana na viambata sumu mbali mbali vya bidhaa hizo.
Aidha
alisema, katika ukaguzi huo wamefanikiwa kukagua ghala la kampuni ya Cross Boda
Treading Company liliopo Tomondo na kugundua takribani ya tani 2.17 za bidhaa mabli mbali mchanganyiko
ambazo zimepitwa na Wakati.
Hata hivyo amewataka wafanyabiashara endapo watakua na Biashara ambazo zimepitwa na wakati wasizitumie bidhaa hizo na badala yake watoe taarifa kwa wakala wa chakula na Dawa ili kuweza kufuata taratibu sahihi za kutekekezwa kwa bidhaa hizo.
Hata hivyo Mkurugenzi Dawa na Vipodozi ametoa wito kwa jamii kuangalia tarehe za mwisho wa bidhaa wanazo zinunua ili waweze kuepukana na madhara mbali mbali yanayoweza kujitokeza ambayo yanasbabishwa na wafanyabiashara wa sio waaminifu.
Miongoni
mwa Bidhaa zilizokamatwa wakati wa Zeozi hilo katika Ghala la cross Boda ni
pamoja ma Mafuta ya kula lita 970, Bia
aina ya savana lita 340, Maharagwe kilo
210,sweatcorn kilo 567, Maziwa ya Maji lita 78 na Tambi zote hizo ni bidhaa
hazifai kwa matumizi ya binaadamu.
No comments:
Post a Comment