Na, Fatma Rajab
Serikali ya SMT na
SMZ zitaendelea na juhudi za kuimarisha dhana ya Ufuatiliaji na Tathmini
kwa pande zote mbili za Muungano hasa katika shughuli za Mipango ya Kitaifa na
Miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na na Mkamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifungua
Kongamano la Tatu(3) la Kitaifa la wiki
ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Mwinyi liliofanyika katika Ukumbi wa
Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege
jijini Zanzibar
Amesem Tanzania inaendele
kupiga hatua katika uimarishaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini ikiwemo
kuweka mifumo na miundombinu yenye kuwezesha utekelezaji wa shughuli za
maendeleo kwa Taasisi za Kitaifa
zinazoratibu masuala hayo kwa maslahi mapana ya nchini
Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe.Hemed amesema matumizi ya Teknoloji katika kufanya ufuatiliaji na
Tathmini kutaiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuimarisha uwajibikaji na kuongeza kasi na uwazi katika kuleta
ustawi wa wananchi kwa kutoa huduma sahihi za kijamii na kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar amesema kuwa anatambua kuwa
mafanikio makubwa yamepatika katika shuhuli za ufuatiliaji na tathmini nchini
hivyo amezitaka Mamlaka husika kufanya jitihada za kukamilisha maandalizi ya
Sera za Ufuatiliaji kwa Serikali zote mbili pamoja na kutenga rasilimali za
kutosha kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini.
Aidha amezitaka Taasisi
hizo kuhakikisha taarifa zinazozalishwa kutokana na kazi za ufuatiliaji
na Tathmini zinatumika katika kufanya maamuzi na kuweka mikakati Imara ya
kuhabarisha Umma juu ya matokeo ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa kushirikiana
na waandishi wa habari ili kufikia malengo ya taasisi na taifa kwa ujumla
Sambamba na hayo Mhe. Hemed
ametowa wito kwa chama cha Wataalamu Afrika ( AFrEA) kuendelea kuvilea vyama
vidogo vidogo vilivyomo nchi wanachama pamoja na kuapta fursa za kujifunza na
kujiimarisha ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratib na Bunge Mhe. William Vangimembe Lukuvi amesema
katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo nchini kunahitaji uwepo wa
taasisi zenye kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ili kusaidia kulinda matumizi ya rasilimali fedha zinazotumika katika miradi
hio.
Mhe. Lukuvi amesema kuwepo
kwa Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza vinaakithi dhamira ya Serikali zote
mbili ya kuhakikisha mabadiliko na marekebisho makubwa yanafanyika katika
kuimarisha Teknolojia na mifumo ambayo itasaidia kufikia malengo yaliyowekwa na
serikali hizo kwa maslahi mapana ya wananchi wa pande zote mbili za muungano.
Akizungumza kwa Niaba ya
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais,
Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amesema kufanyika kwa Kongamano la
Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza hapa Zanzibar litaibua na kupendekeza njia
nzuri zaidi za kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini hasa katika masuala ya Utalii
na Uwekezaji nchini
Mhe. Sharif amesema
kufanyika kwa Ufuatiliaji na Tathmini kunasaidia katika kupima shuhuli za
mipango ya maendeleo ya Kimataifa, kitaifa na Kikanda kwa kutathmini ufanisi na
uwajibikaji wa Taasisi husika hasa katika kupata taarifa na Takwimu sahihi
zenye matokeo chanya ya mipango hio.
No comments:
Post a Comment