Wananchi wa Shauriwa kuunga Mkono juhudi Za Serikali Kutunza Miundombinu

 


 Na, Mwandishi wetu

Jamii imeshauriwa kuunga Mkono jihudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi katika  sehemu mbalimbali  nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe, Hamza Hassan Juma  ametoa kauli hiyo Kizimkazi Dimbani wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jmaii TASAF Kwa Upande wa Zanzibar.

Amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  ndio waratibu na wasimamizi wa miradi mbalimbali ya Muungano ambayo inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jmaii TASAF  ambayo imekuwa ikisaidia wananchi  katika maeneo mbalimbali ya nchi

Alisema kuwa, Miradi ya elimu, Afya na ujenzi wa Miundombinu ya Barabara imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya wananchi hivyo nivyema wananchi kupitia maeneo yao kuitunza na kuiendeleza miradi hiyo ili iweze kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, Waziri Hamza. ameendelea Kuwaasa wananchi na wahusika wa Miradi hiyo  kuenedelea kuitunza kwani miradi hiyo imeharimu fedha nyingi za Serikali na inanufaisha wananchi wengi kwawakati mmoja.

Akizungumza katika Ziara hiyo mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji. ameeleza kuwa Miradi hiyo imeharimu fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kwenda kwa wananchi.

Ameeleza kuwa jumla ya Tsh  215,000,000.zimetumika katika  ujenzi wa kituo cha Afya Upenja, na jumla ya Tanzania Tsh 117,000,000.zimetumika katika ujenzi wa  ukumbi wa mkutano  Skuli ya Bambi huku jumla ya Tsh  291.1 zimetumika katika Ujenzi wa  Dahalia ya wanawake Skuli ya Kizimkazi Dimbani.

Katika hatua nyengine mratibu  ameeleza kuwa miradi hiyo ambayo imejengwa kwa mashirikiano makubwa kwa nguvu za wananchi inakaribia kumalizika na kukabidhiwa kwa sekta husika kama ilivyo kubaliwa katika sheria.

Kwa Upande wake muhandisi kutoka wizara ya Afya  ameleza kuwa miradi hiyo imejegwa kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya wanachi na tayari imefikia aslimia 75% kukamilika kwa wakati ulio pangwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Mzee Ali Mohamed Mrisho. mkaazi wa Bambi alieleza kuwa wanafurahishwa na kuridhishwa na kazi inayofanywa na Serikali zote mbili katika utekelezaji wa maradi na ujenzi wa ukumbi wa Mitihani katika eneo loao ambapo kabla yahapo walikuwa  wakipata tabu kuwaweka wanafunzi kufanya mitahani katika darasa moja.

jumla ya miradi mitano imetembelewa katika ziara hiyo ikiwemo kituo cha Afya upenja,ujenzi wa ukumbi wa mitihani Bambi, Ujenzi Dahalia ya wanawake kizimkazi Dimbani ,ukarabati wakituo cha Afya kwa Mtipura pamoja na Ukarabati wa Skuli ya maandalizi Mkele.


1 comment:

Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar

Na, Mwandisho.   Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowa...