Na, Mwandishi wetu
Wajasiriamali
wanaonufaika na mradi wa maendeleo ya
Jamii TASAF wameishukuru serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia
mradi wa Tasaf kwa kuwawezesha kushiriki
maonesho ya nane nane yanayoendelea Dole
wilaya ya Magharibi A ambayo yamewaongezea fursa mbalimbali za kiuchumi na Biashara.
Wametoa kaulihiyo Mapema leo huko Dole wakati walipokuwa wakifanya mahojiano na kueleza mafanikio waliyoyapata kutokana na uwepo wa maonesho hayo ya nanenane ambayo yametoa fursa ya kuuza bidhaa Zao na kujitangaza kibiashara.
Akitoa
Ufafanuzi juu ya ushiriki wa walengwa hao wa Mpango katika Maonesho hayo Afisa
Ufuatiliaji Zanzibar, Ramadhani Madar. amesema kuwa TASAF imekuwa ikwashirikisha walengwa kutoka
Unguja na Pemba katika Maonesho mbalimbali kwa lengo la kujitangaza na Kuuza Bidhaa
wanazo zizalisha ili kupata Masoko na kujiendeleza kiuchumi.
Madari
ameeleza kuwa, Lengo la TASAF ni kuwatafutia Masoko ya Kuuza Bidhaa Mbalimbali wanazo zizalisha kupitia vikundi vyao ambavyo vimekuwa msada mkubwa wakupata
maendeleo na kufikiwa lengo la TASAF.
wajasiriamali wa TASAF wakiuza Bidhaa zao kwa wageni katika Maonesho ya nanenane Dole
Aidha
wajasirimali hao wamesema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia TASAF imekuwa ikiwawekea
mazingira wezeshi ya Kushiriki maonesho ambayo yamekua chachu ya kupata masoko
ya Bidhaa zao. ameleza Mzee Hassan.
Ameeleza kuwa, kwa sasa nimefikia ukomo wakuwa mwanakaya lakini naishukuru serikali kwakuniwezesha kuendesha maisha yangu kupitia fedha za TASAF na kupitia biashara ndogondogo tunazo ziendeleza.
Kwa
Upande wake Bi.Mariayam Kassim Abdallah. amesema uwepo wao katika maonesho hayo
wamepata kujifunza namna ya kutengeneza
bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali wengine jambo ambalo
limewafanya kuzitangaza biashara zao kwa wananchi wengine kwa Urahisi.
Nae,
Raya Sulieman Hamadi, kutoka Kaskazini pemba ambaye ni mnufaika wa TASAF ameeleza
kuwa amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na TASAF kuwapeleka katika Maonesho
kama hayo amabayo yamekuwa na Msada mkubwa kibiashara.
Moenesho
hayo ya nane nane ambayo ni ya saba yenye kauli mbiu ya ‘’Kilimo ni utajiri
kila Mtu atalima’’ yanatarijiwa kufungwa kesho katika viwanja hivyo vya Dole .
No comments:
Post a Comment