Jamii ya Shauriwa kutunza Mazingira ili kurithisha Vizazi vijazo

 


  Na, FATMA  RAJAB


Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo umwagiliaji  maliasili na mifugo zimeanzisha mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijani (The Green Legacy Zanzibar) lengo ikiwa ni kuifanya  Zanzibar kubaki  katika hali yake ya ukijani wa asili.

Hayo yameelezwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman. katika uzinduzi wa mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijani uliofanyika Nyamanzi mkoa wa magharibi Unguja.

Alisema kupitia hali ya kijani  Serikali ilianzisha mipango ya kupanda na kuhifadhi miti tangu mwaka 1964 pamoja na kuendeleza juhudi mbali mbali zilizochukuliwa miaka ya nyuma za kuhifadhi misitu.

Aidha, alisema mpango huo unakusudia kuwashirikisha na kuwaleta pamoja wadau mbali mbali kutoka sekata na ngazi zote kupanda na kuitunza miti ya aina zote.

Aidha alisema kuwa, mpango huo una kusudia kuongeza hamasa kwa kila mtu kushiriki kikamilifu pamoja na kujenga jamii yenye utamaduni na tabia endelevu ya kuthamini, kupanda, kutunza miti na kuepuka kukata miti ovyo ili kuepusha athari mbali mbali ambazo zinaweza kujitokeza kwa kukatwa kwa miti.

Mhe, Makamu alisema kuwa, mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijani umekuja mara baada ya kuona kuwa kumekuwepo  na mambo mengi ambayo  yanasababisha  upoteaji mkubwa wa miti na misitu  kutokana na shughuli mbali mbali za kibinaadamu  pamoja na ukuaji wa miji ambayo ujenzi wake unachukuwa eneo kubwa  la ardhi Kutokana na  ongezeko la idadi ya watu pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Sambamba na hayo alisema mpango huo pia umeanzishwa kuhsmasisha na kuwawezesha wananchi wa Zanzibar pamoja na watu mbali mbali  kuelewa umuhimu wa misitu na kuihifadhi miti iliyopo kuipanda na kuitunza ili kuimarisha mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.


Nae, waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda Mhe, Omar Said Shaabani. alisema mpango wa uhamasishaji upandaji wa miti katika jamii ni sehemu ya misha ya viumbe hai hivyo jamii inatakiwa iwe na utamaduni wa kuyaenzi na kuyatunza mazingira kila wakati kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

"Tutaendelae kushirikiana vizuri na wizara ya elimu na mfunzo ya amali ili kuhskikisha kuwa wanawafundisha wanafunzi wa Sekondari na vyuo vikuuu kujua umuhimu na thamani ya upandaji wa miti kuweza kufikia dira ya mpango huo.

Kwa upande wake Mstahiki meya Mhe, Mahmoud Mohammed Mussa. ameeleza kuwa serikali kupitia youth climatic fund imezitaka Taasisi na mashirika mbali mblia kwa ujumla na kuhamasisha utunzaji wa miti na kutunza mazingira muda wote."mpaka sasa tumepanda miti isiyopungua elfu kumi kwa upande wa visiwa vya unguja na pemba ambapo mradi wa youth climatic umefikika katika ushindani wa kutafuta vikundi vitakavyofanya kazi katika kuwezesha upandaji wa miti elfu tatu. 3,000,000.

Mpango huo utainufaisha jamii ya Zanzibar kwa kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi na hasara nyengine za kimazingira, ambao umekuwa na kaulimbiu isemayo "Zanzibar ya kijani inawezekana shiriki kupanda na kutunza miti".


No comments:

Post a Comment

ZSTC yaridhiishwa na Chuo cha Mafunzo Katika Uimarishaji wa Zao la Karafuu

  Na. Mwandishi Wetu. Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Nd. Soud Said Ali amesema Shirika la Biashara Z...