Na, Mwandishi wetu
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amewataka watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya wananchi zinalindwa na kutumika ipasavyo ili Watanzania waendelee kunufaika na Mfuko huo
TASAF uliofika Ofisini
kwake Vuga kwa lengo la kujitambulisha.
Amesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF umekuwa ni mkombozi kwa Watanzania walio wengi hasa wanyonge hivyo uongozi huo una jukumu kubwa la kuhakikisha unadhibi na kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za mfuko huo.
Makamu wa Pili wa Rais
ameutaka Uongozi huo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF SHEDRACK MZIRAY kulipa kipaombele suala la utoaji wa Taaluma
kwa wanufaika juu ya Dhamira na Malengo ya mfuko huo ili kupunguza malalamiko
kwa wanufaika hao mara tu wanapomaliza ama kukosa sifa za kuendelea kunufaika na
huduma zinazotolewa na TASAF.
Aidha Mhe. Hemed amesema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoka mashirikiano makubwa kwa watendaji wa TASAF wa Pande zote
mbili za Muungano ili kuhakikisha Watanzania wanaendelea kunufaika na mfuko huo
na malengo ya Viongozi wakuu wa Serikali ya kuwaondolea changamoto mbali mbali
wananchi wake yanafikiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndugu SHEDRACK MZIRAY amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo na maagizo yote waliyopatiwa na Makamu wa Pili wa Rais kwa kuendelea kudhibiti Nidhamu katika matumizi ya fedha, Nidhamu kwa watendeji wa mfuko huo na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya kuwepo kwa mfuko huo nchini.
MZIRAY amesema Tasaf
imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na kwa mashirikiano mkubwa na Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar hivyo anaamini kuwa
ushirikiano huo utaendelea kudumu
katika kipindi chote cha Utumishi wake na kuahidi kuwa Matunda ya Mfuko huo
yatawafikia na kuwanufaisha wananchi wa
pande zote mbili za Muungano.
No comments:
Post a Comment