Na, Mwandishi wetu.
Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema wapo kwenye mchakato wa kuunda kamati
maalumu ya kutafuta fedha kuongeza fedha za ufadhili kwa ajili ya wanafunzi
wanaosoma masomo ya sayansi, uhandisi na elimu tiba nje ya nchi.
Profesa Mkenda ametoa kauli
hiyo leo Agosti 24, 2024 wakati akizindua bweni la wasichana, vyumba vya
madarasa na maabara Sekondari ya Kizimkazi Dimbani ambavyo vimejengwa na Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Katika hafla hiyo, Waziri
Mkenda amesema serikali inaendelea kuhamasisha wanafunzi wengi wajitokeze
kusoma masomo hayo kwani hakuna taifa linaweza kuendelea kama halina wataalamu
katika sekta hizo.
Amesema tayari serikali
imeanzisha mfuko maalumu wa Samia Scolaship ambapo mwanafunzi katika maeneo
hayo anapata ufadhili na serikali kwa asilimia 100 na kugharamiwa kila kitu
anapkwenda nje kusoma.
“Kuna fursa nyingi za kusoma nje ya nchi hatuwezi kujifungia ndani kisha tukategema kuendelea hata mataifa yaliyoendela yasomesha watu wake nje, kwahiyo tuchangamkie fursa hii,” amesema
Waziri Elimu,Sayansi na Tekenolojia Prof. Adolf Mkenda (MB) akizungumza katika Uzinduzi wa Dahalia ya Waschana Kzimkazi Dimbani Ulio jengwa kwa Fedha za TASAF
“Tumeshatenga fedha lakini
tunataka kuunda kamati maalumu ya kutafuta fedha kwa kushirkiana na mabenki ili
kuongeza mfuko huo kuwasaidia wanafunzi kusoma,” amesema
Ametumia fursa hiyo kuwataka
walimu, wazazi kuwahimiza wanafunzi kusoma masomo hayo kuanzia kidato cha kwanza
ili wanufaike na fursa hiyo.
Kwa mujibu wa Profesa Mkenda amesema wakati wanaanzisha ofisi ya Atomu Zanzibar walitafuta watu wenye sifa lakini wamebaini kuna chngamoto kubwa ya watu wenye elimu hiyo hivyo wameanza mpango kuwekeza katika eneo hilo kuwasomesha watu wenye sekta hiyo.
Amesema wameagiza sasa
itengwe bajeti katika taasisi hiyo kwa ajili ya kusomesha wataalamu hao.
“Kwahiyo mtaona kuwa kuna fursa nyingi yapo maeneo ambayo tunahitaji wataalamu lakini hatuna wa kutosha tutumie fursa hii,”
Mkurugenzi Mkuu wa Tasaf
Shadrack Mzirai amesema katika kipindi cha pili cha uhaulishaji wa fedha kwa
kaya masikini jumla ya Sh48.84 bilioni zimetolewa kwa kaya 53,441.
Amesema zaidi ya miradi 761
yenye thamani ya Sh15 bilioni imeibuliwa kati ya kiasi hicho, Sh1.98 bilioni
zimetumika kununua vifaa huku Sh13 bilioni zikitumika kulipa ujira kwa wananchi
wanaoshiriki kujenga miradi hiyo ambao wanatokana na kaya hizo zinazonufaika na
mfuko.
“Katika miradi iliyoibuliwa
ni pamoja na barabara, ujenzi wa shule, mazingira uvuvi na miundombinu hivyo
wananchi hao kujiongezea kipato kile kinachotokana na mfuko wenyewe.
Amesema kupitia mpango huo
wamenzisha vikundi vya ujasiriamali mbapo zidi ya wananchi 23, 000 wamenufaika.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali, Khamis Abdalla Said amesema vyumba vinne vya madarasa
vyenye uwezo wa kubeba wanafunzi 180 sawa na wastani wa wanafunzi 45 kila
darasa.
Kwa mujibu wa katibu Mkuu
maabara na vyumba hivyo vimegharimu zaidi ya Sh400 milioni.
Hatahuvyo amesema Serikali
inaendelea kuhakikisha inaondoa changamoto za elimu na wanafunzi wasisome
mikondo miwili.
No comments:
Post a Comment