Madakari Ngazi ya Awali Kupatiwa Elimu kuhudumia wangonjwa Mahututi

  Na.Mwandishi wetu.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema hatua ya kuwajengea uwezo watoa huduma wa vituo vya Afya vya msingi juu ya namna bora ya kutoa huduma ya awali kwa wagonjwa mahututi kabla ya kufikishwa hospitali kubwa kutaweza kuokoa maisha ya wananchi wengi nchini.

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Huduma ya Dharua na wagonjwa mahututi katika Ukumbi wa Hotel ya Verde Zanzibar.

Amesema kuwa Tafiti zinaonesha kuwa baada ya kuanzishwa mifumo ya utoaji wa huduma za dharura imesaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa vifo na vilema vitokanavyo na majanga  hivyo ni lazima  kuzidi kuimarishwa kwa mifumo hio kuanzia katika ngazi ya jamii ili kuweza kudhibiti kasi ya vifo vitokanavyo na majanaga.

Rais Dkt.Mwinyi amesema Tanzania kama nchi nyengine duniani hatuna kinga ya kutokupata dharura hasa ya majanga mbali mbali yakiwemo ajali za barabarani, baharini, vimbunga, magonjwa yasiyo ya kuambukiza na magonjwa yakuambukiza ambayo yamekuwa yakipoteza maisha au kuacha vilema vya kudumu ambavyo vinategemea msaada mkubwa kutoka kwa kada ya magonjwa ya dharura kuweza kupambana na magonjwa hayo.

Dkt. Mwinyi amesema katika kuimarisha huduma za dharura na wagonjwa mahtuti Serikali imejenga na kuzifunga hospital 10 za Wilaya na Mkoa ambazo zina miundombinu na vifaa tiba kwa ajili ya kutoa huduma za tiba za dharura pamoja na kuzindua kituo cha uendeshaji wa huduma za dharura za afya ya jamii Zanzibar chenye lengo la kubaini na kushuhulikia kikamilifu vitishio vya Afya ya jamii Zanzibar

Sambamba na hayo Dkt Mwinyi amesema Serikali imefanya ukarabati mkubwa na kuweka vifaa na mifumo ya TEHAMA katika kituo cha huduma ya dharura na Afya ya jamii (Afya Call Center) kilichopo Magomeni kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata elimu ya Afya na msaada wa haraka wanapofikwa na dharura za kiafya kwa kupiga simu bila ya malipo.

Ameupongeza Uongozi wa Akademia ya huduma za dharura (EMSA) wadau na vyama vyengine vya kitaaluma kwa kushirikiana na Serikali kusambaza huduma za dharura nchini na kuwahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango wao na inafarijika kuona juhudi zinafanyika za kuona maendeleo makubwa ya ya utoaji huduma bora ya dharura na wagonjwa mahtuti hapa Zanzibar.



Nae waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazurui amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti katika kukabiliana na majanga mbali mbali na kutokomeza kabisa ulemavu na vifo vinavyoweza kuepukika.

Mhe. Mazrui amesema kuwa uwepo wa  mifumo Imara na endelevu ya kutoa huduma ya tiba ya dharura na wagonjwa mahtuti kwa wakati kutapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto na hata majanga yatokanayo na ajali mbali mbali ambayo yanaendelea kugharimu maisha ya wananchi wengi.

Amesema licha ya uhaba wa madaktari bingwa wanaoshuhulikia utoaji wa huduma za dharura na wagonjwa mahtuti bado jitihada ya makusudi zinahitajika kutoka katika kitengo cha Imajensi na vitengo vyengine vya tiba kwa kufanya kazi kwa kushirikiana katika kutoa matibabu ya haraka kwa wananchi ili kuokoa maisha ya wananchi wengi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Akademia ya Huduma za Dharau (EMSA) Dkt. SILIVESTA FAYA amesema lengo la kuwepo kwa kongamano hilo ni kuwapatia Taaluma watendaji wa Wizara, Taasisi na Wadau wa Afya juu ya utowaji wa huduma za tiba ya dharura na wagonjwa mahtuti hasa katika ngazi ya huduma ya Afya ya msingi.

Dkt. FAYA amesema  EMSA imejipanga kuleta mageuzi makubwa ya Utowaji wa Huduma za Dharau kwa kuwajengea uwezo na kuwapatia ujuzi na vifaa tiba watoaji wa huduma hio ili kuweza kufanya kazi zao kwa uweledi na kwa wakati jambo ambalo litasaidia  kuokoa maisha ya Watanzania.


No comments:

Post a Comment

Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar

Na, Mwandisho.   Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowa...