Wananchi watakiwa Kufuata Sheria Sahihi Za Matumizi ya Ardhi

 

Na, Fatma Rajab



Wananchi wametakiwa kua na matumizi  mzuri ya Ardhi ili waweze kuepukana na changamoto mbali mbali ambazo zinaweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na waziri wa ardhi na maendeleo ya makaazi Mhe, Rahma Kassim Ali katika Ghafla ya uzinduzi wa utoaji hati miliki za Ardhi za kilimo (eka tatu)  iliofanyika katika ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.

Alisema ni vyema kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka husika pindi wanapotaka kubadilisha mashamba yao kutoka kwenye matumizi ya kilimo na kwenda kwenye matumizi ya makaazi ili kuweza kupata mabadiliko ya hekta yaliokuwa sahihi.

Aidha alisema, anawatak wananchi kuacha tabia ya kukata na kuuza maeneo  bila ya kufuata taratibu wakati wa kukatiwa viwanja hivyo na serikali kuchukuwa asiimia ndogo lengo ikiwa ni kuwashajihisha wananchi kuacha tabia ya kubadilisha matumizi binafsi na kuweza kuepusha matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake katibu mtendaji kutoka kamisheni ya Ardhi Mussa Kombo Hamad. alisema baada ya muda mrefu kutokuwepo kwa zoezi la utoaji wa hati miliki sasa wameamua kutoahati hizo zenye lengo la kuhamasisha wananchi mbali mbali wanaomiliki mashamba ya eka tatu kukamilisha taratibu za kupatiwa hati ya matumizi ya mashamba yalio sahihi.

Aidha alisema wanampngo wa kuendesha zoezi la kuhakiki maeneo ambayo yanafaa kuwa ni ya heka na kujua ni  mashamba gani ambayo yamepotea kuwa ni mashamba ya eka

"Tunafahamu kwamba hili ni zoezi muhimu na kwasababu ya umuhimu wa ardhi   kwa ajili ya kilimo na jambo ambalo limeasisiwa toka mapinduzi hivyo ni vyema kuliendeleza na kusimamia vizuri mashamba hayo ili yaweze kudumu kwa vizazi vya sas na baadae"

Aidha,aliwataka wananchi wenye mashamba ya kilimo ya Serikali wafike kamisheni ya Ardhi ili kuweza kupatiwa hati zilizo Rasmi ambazo zitasaidia kuondosha migogoro mbali mbali inayoweza kujitokeza.

Kwa Upande wao wananchi waliokabidhiwa hati hizo  walisema  wanaishukuru serikali kwa kuwapatia nyaraka hizo kwani kumepunguza changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zikijitokeza.

Hivyo ni vyema wananchi kufuata taratibu zilizowekwa kwa Ardhi ni mali ya watu wote na ni vyema kuitunza ili iweze kudumu kwa vizazi vya sas na vijavyo na zoezi hilo lilo ambatana na hati miliki ambazo ni halali kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar

Na, Mwandisho.   Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowa...