Na, Mwandisho.
Unguja.
Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
wameeleza namna mpango huo ulivyowaondoa kuitwa kaya masikini na sasa wanaweza
sio tu kujitegemea bali wamekuwa msaada kwa watu wengine.
Mpango
wa kunusu kaya masikini kwa Zanzibar ulianza mwaka 2013 ukiwa katika afua tatu:
Ruzuku, ajira za muda na miundombinu ambapo mpaka sasa ina vikundi 3,372 vyenye
wanachama 45,948.
Vikundi
hivyo vimekusanya akiba ya zaidi ya Sh1.6 bilioni na vimeendelea kukopeshana
kwa ajili ya kuanzisha na kutekeleza miradi ya kuwaongezea kipato.
Wakizungumza
katika maonyesho ya biashara ya kimataifa Dimani Nyamanzi Januari 13 2025,
baadhi ya wajasiriamali wanaonufaika na mfuko huo wamesema hawakuwahi kufikiria
kama wanaweza na wao wanweza kushirkia maonyesho makubwa ya biashara kama hayo.
Khadija
Slaym Salim mkazi wa Kianga amesema mwanzo walikuwa kaya masikini lakini
kwasasa wanajivunia kunufaika wamenufaika kupitia kwenye vikundi vyao na
kujiongezea vipato.
“Ukiachilia
mbali kuwa kwenye vikundi lakini kila mtu nyumbani kwake anaedesha biashara
zake binafsi mimi nyumbani ninamlango wa duka kila ninachopata naongeza, Tasaf
imetunufaisha tunaweka akiba ikifika mwisho wa mwaka tunagawana zingine
tunaacha kuendeleza biashara zetu,
Khadija mesema mbali na kunufaiaka mmojammoja lakini wamenufaika kwenye huduma za kijamii kama shule, barabara, na hospitali kwasasa watoto wanakwenda shuleni bila changamoto zozote
“Tofauti
na mwanzo watoto walikuwa wanashindwa kwenda shule, mikoba ya daftari hawakuwa
nayo, mtoto akienda shule tulikuwa tunakunguta mifuko ya unga tunawapa lakini
sahiv begi wanapata,” amesema
Amesema
huu mpango walioleta umesaidia wanawake kwani kipindi cha nyuma ilikuwa lazima
mpaka wategemee wanaume lakini kwasaa wanajitegemea wenyewe na kuwasaidia
wengine.
Ametumia
fursa hiyo kuwasihi wanawake wanapopata fursa kama hiyo kijiendelza kwenye
vikundi ili wazidi kujikwamua kimaisha.
Mnufaika
mwingine, Naomba Bakari Hassan kutoka Kikundi cha Kutoa ni moyo Chakechake
Pemba amesema walikuwa na maisha magumu lakini kwasasa wanaendelea kuimarika
kupitia kwenye vikundi vyao.
“Sasahivi
tunasomesha watoto tunapata fedha za huduma za nyumbani na kusomesha watoto
tofauti na ilivyokuwa awali tunashukuru tunapata kwasaa tumeondoka kwenye
utegemezi, kwasasa kila kitu tunaweza kufanya wenyewe na tumeimarika,” amesema
Naomba
Amesema
kabla ya kuingia kwenye mradi alikuwa na maisha magumu lakini kwasasa ni maisha
bora, “familia yangu inakula, namimi najitosheleza mahitaji yangu kupitia
biashara ninayoifanya.
Naomba
anayefinyanga viotezo na kushona mikoba anasema ndoto zake anataka awe
mfanyabiashara mkubwa na kuwa na maisha bora zaidi.
Mwingine
mtoto wa mnufaika Raya Suleiman Hamad kutoka kukindi Tushikamane cha Mgogoni
Wete Pemba anasema wazazi ndio wapo kwenye mpango walipopata ruzuku
wakatengeneza mafuta na bidhaa zingine kwa ajili ya kuuza.
Raya
ambaye amesomeshwa na ruzuku ya Tasaf iliyokuwa ikitolewa kwa wazazi wake,
amesema kwasasa ameshakuwa mtaalamu kwenye ujasiriamali baada ya kufundishwa
hivyo wanataka kufika mbali zaidi kwenye maisha.
Mkurugenzi
wa Mifuo na Mawasiliano ya Umma Tasaf, Japhet Boaz amesema hizi zilikuwa kaya
masikini ambazo hazikuwa na uwezo kujitokeza ila kwasasa wameugana pamoja na
wanatengeneza bidhaa na kuja kwenye maonesho kama haya ya kimataifa.
“Wametumia
faida kuwapeleka watoto shule, na kujiwekea akiba wakifanya mambo mengi ya
maendeleo na kuimarisha makazi yao na kuwekeza mengine,” amesema
Kwa
mujibu wa Boaz, wanatiwa moyo kwamba kazi wanayoifanya na kazi ambayo serikali
imedhamiria kwa wanachi wake inaleta matunda.
Amesema kaya baada ya kuzisaida wanaziweka kwenye vikundi, wanaweza kuweka akiba na wanaweza kukopeshana eneo ambalo nalo linafanya kazi vizuri.
“Kiasi
kwamba hata hawa tunaowaona hapa kwenye maonyesho wametoka kwenye vikundi
wakabuni miradi kulingana na mazingira waliyonayo kisha wameendelea kutengenza
vitu mbalimbali na bidhaa nyingi zinazotokana na asili,” amesema
Kwa
upande wa Zanzibar kuna afua tatu, wanatoa ruzuku ya fedha kwa kaya masikini
ambapo mpaka sasa wameshatoa Sh50.1 bilioni kwa muda wa miaka 10 kwenda kwenye
kaya masiki.
Afua
ya pili wanatoa ajira za muda kwenye kaya hizo ili kuwaongezea kipato wanabuni
miradi katika jamii wanafanya kazi wanapata ujira unaowasadia kuongeza kipato.
Afua
nyingine ni ujenzi wa miundombinu ambapo katika hilo wanaangalia eneo ambalo
linapungukiwa katika sekta ya elimu, afya pamoja na maji.
Amesema
Tasaf imekuwa mstari wa mbele kuitikia wito wa serikali ambapo katika sherehe
hizi za Mapinduzi wamezindua vituo vya afya viwili, Upenja Kaskazini Unguja
ambachokitahudumia zaidi ya wananchi 1100 na Kingine kipo Wete Pemba Kinyikani
na nyumba ya watumishi.
Amesema
wameona kuna upungufu wa huduma za jamii kwahiyo kaya masikini wanazohudumia
inakuwa ni ngumu kufuata huduma hizo kwahiyo inawaletea athari kubwa.
Amesema
wanaamini kaya nyingi pamoja na jamii nyingine watapata huduma katika maeneo
waliopo kwa ufanisi zaidi.
Naye
Mratibu wa Tasaf Unguja, Makame Ali Haji amesema kwa taratibu za Tasaf kila
kikundi kinakuwa na wanachama 15 ambao wanajiweka pamoja kujiweka akiba na
kuanzisha biashara ndogondogo, “tunashukuru wametumia rasimali za bahari
kujiendeleza kiuchumi”
“Wapo
wanaolima mwani na wengine wameanzisha uzalishaji wa sabuni unaotokana na
mwani, tunashukuru sana wananchi hawa wameweza kujiimarisha kiuchumi na
tunafahamu mpango huu unaendelea vizuri,” amesema Makame
Amesema
walengwa hao ni kwamba wametoa katika mpango wa masikini na kutafuta wengine
wapige hatua wajiendeleze na kujikwamua kiuchumi.
.
Ni jambo la kujivunia
ReplyDelete