Na, Fatma Rajab
Baraza
la sanaa, sensa ya filamu na utamaduni, (BASSFU) limezuia upigwaji wa mzuki
katika maeneo ya baa zote ndani ya Zanzibar
ambazo hazina maeneo maalum ya kuzuia sauti (soundproof) ili kuepusha
usumbufu unaosababishwa na sauti ya
muziki kwa watu mbali mbali ikiwemo wanaofanya ibada, watalii, wagonjwa,
wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Hayo
yameelezwa na katibu mtendaji baraza la sanaa,
sensa ya filamu na utamaduni Chuom Juma Chuom wakati alipokuw
akizungumza na waabdishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa studio ZBC raha leo zanzibar
Amesema
"uamuzi haukuja kwamba tumeamua kuzuia sanaa bali lengo la uamuzi huu ni
kutaka jamii ibaki salama dhidi ya maudhi yanayotokana na sauti za upigaji wa
mziki katika maeneo ya mabaa ambapo watu wa ibada wwfanya biashara mbali mbali
ikiwemo biashara ya utalii, wanafunzi ambao wapo katika mskuli mbali mbali
lakini pia na jamii kwa ujumla imekua ikiathirika kutokana na upigaji wa mziki
kiholela".
Lengo
jengine la uamuzi huo ni kutaka kuweka ustawi mzuri wa jamii amesema"
hatuna dhamira mbaya ya kukwaza shughuli za sanaa na burudani tunataka sana, tunapenda
sana serikali yetu inayoongozwa na raisi dkt hussein ali mwinyi na waziri wa
habari sanaa utamaduni na michezo ni wapenzi wa sanaa na burudani lakini kwa
vile kuna wananchi wanaoongoza tunachotaka kwa pamoja ni kutoa fursa kwa sanaa
na burudani yenye kufuata maadili mila desturi na ustawi wa kijamii".
Aidha
amesema baraza la sanaa limejipnga kwa kushirikiana na vyombo mbali mbali vya
serikali ikiwemo jeshi la polisi, afisi za wakuu wa wilaya, masheha
,wakurugenzi wa manispaa pamoja na halmashauri kuhakikisha wanadhibiti baa
ambazo zinapiga mziki usiozingatia taratibu na sheria zilizopangwa ikiwemo za
kuwepo maeneo maalum ya kudhibiti sauti.
Hata
hivyo amesema baraza la sanaa halitatoa leseni katika maeneo ya mabaa ambayo
hayana maeneo maalum ya kudhibiti sauti (soundproof)"kwa maeneo
ambayo tayari yameshahenga maeneo ya
soundproof tutaendelea kutoa leseni katika maeneo hayo lakini pia tutaendelea
kuyasimamia kufanya shughuli za sanaa na
burudani kwa misingi ya taratibu, sheria kanuni na miongozo mbali mbali
ambayo ipo na tunaendelae kuwapatia".
Hiyvo
baraza la baraza linaendelea kufanya ziara za ukaguzi katika maeneo yote ya
burudani kwa lengo la kudhibiti athari zinazotokana na kelele za muziki kwa
jamii," sisi baraza la sanaa kwa kushirikiana na mamlaka ambazo tumezitaja
kesho tutafanya operesheni kali ya kudhibiti na kuchkukua hatua kali kwa
taasisi ama mtu yoyote ataekwenda kunyume na taarifa hii".
No comments:
Post a Comment