Na, Fatma Rajab.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimekuwa zikichukuwa hatua mbali
mbali kuweza kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya
tabia ya nchi miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuingiza mabadiliko ya tabia
ya nchi kwenye mipango ya Taifa ya maendeleo kama vile dira ya Taifa ya maendeleo ya zanzibar ya
mwaka 2025 na mpango wa maeneleo ya zanzibar wa 2021 2026..
Hayo yameelezwa na waziri
wa nchi afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman wakati
alipohudhuria mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabia ya nchi uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh
Idrissa Abdul wakil kikwajuni Zanzibar,
Amesema serikali imetaarisha mkakati wa mabadiliko ya Tabia ya nchi wa zanzibar wa mwaka 2014 ambao umeeleza vipaumbele na hatua zinazofaa kuchukuliwa na kukabiliana na mabadiliko hayo kuwepo kwa hatua mbali mbali za kupanda miti ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na miti ya mikoko, mitandaa katika maeneo ya fukwe ili kupunguza kasi ya uingiaji wa maji ya bahari katika maeneo ya kilimo kwa lengo la kuwafanya wananchi wetu kuendelea kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kilimo na kiuchumi"
Aidha amesema katika kipindi
cha miaka 30 iliyopita wastani wa kiwango cha joto kilipanda ongezeko kubwa la
kiwango cha juu cha joto kufikia nyuzi joto 39" hivi karibuni imeshuhudia mvua zisizotambulika
wakati mwengine zinanyesha kubwa na kupelekea mafuriko wakati mwengine
zinanyesha kinyume na wakati tusioutarajia haya yote ni yanatokana na athari ya
mabadiliko ya tabia ya nchi,.
Aliongeza kusema kuwa maeneo ya ukanda wa pwani yaliyochini ya
muinuko wa mita 5 yapo kwenye tishio la
kuathirika na kupanda kwa kina cha bahari na maeneo hayo kwa unguja yanajumala
ya kilomita za mraba 328 na kwa kisiwa
cha pemba yana kilimita za mraba 286.
Kwa mujibua wa taarifa zilizokusanywa na na afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais mwaka 2012 Zanzibar ina jumala ya maeneo 148 yakiwemo pemba 123 na Unguja 25 yanaingia maji ya chumvi na zaid yakitumiwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi, kilimo kijamii lakini kutokana na kuingia maji ya chumvi yanayosababisha kupanda kwa kina cha bahari wananchi wa maeneo hayo sasa hawawezi tena kuendelea na shughuli zozote katika maeneo hayo
Aikizitaja sekata za
kiuchumi zilizo athirika zaidi na mabadiliko ya Tabia ya nchi Mhe Harusi
amesema"sekata za kiuchumi zilizoonekana kuathirika zaidi hapa Zanzibar ni uvuvi wa ukanda wa pwani, ukulima
wa mwani ,kilimo ,utalii,maji makaazi na miundombinu".
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa
jumuiya ya Zanzibar Climate Change alliance ZACCA ambae pia ni mwenyekiti wa
mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabia ya nchi Mahfoudh Shaaban amesema kuna tathimini ambazo
wamezifanya wao kama zacca kwa kushirikiana na wadau wengine ni kuweza
kuchunguza uwelewa na ufahamu lakini pia ni kutaka kujua ni naman gani ya wadau
mbali mbali kuanzia serikali mpaka wadau wa asasi za kiraia wanaweza kuhimili
athari za mabadiliko ya tabia y nchi.
Hatahivyo amesema kuwa tathimin
hiyo imeonesha kuna uwazi mkubwa wa watu kuelewa masuala hayo hivyo mkutana huo
una lengo la kujenga uwelewa wa kuendeleza na kuimarisha nguvu za pamoja katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabia
ya nchi hapa Zanzibar.
Inabidi hatuw za maksudi zichukuliwe
ReplyDeleteSafi
ReplyDelete