Na Fatma Rajab
Waziri wa Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee, na Watoto Zanzibar,
Mhe. Anna Athanas Paul amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto inamuonesha kuwa
na haki ya kucheza Michezo ya aina yoyote hivyo ameitaka Jamii kuunga mkono
juhudi za Watoto katika harakati za kujijengea uwezo kupitia michezo.
Akizungumza mara baada ya
kushuhudia Michezo ya Watoto katika Viwanja vya Mou Tes Tung amesema, Wizara
hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar wataendelea kuunga mkono
shughuli za michezo kwa Watoto na kuwalinda katika nyanja zote za maisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Jumuiya za Michezo zilizochini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hashim
Pondeza amesema, Wanawake wanapaswa kushiriki katika Michezo kwa misingi ya
mila na desturi, hivyo ameitaka Jamii kuendelea kuwahamasisha Watoto kushiriki
katika Michezo mbalimbali ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uelewa na
kujiamini katika harakati zao za kila siku.

Kwa upande wake Afisa
Programu kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA
ZNZ Asia Hakim Makame amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika
kuelimisha jamii, umuhimu wa mtoto wa kike kushiriki katika michezo na kufikia
ndoto zao.
Maadhimisho hayoya siku ya
mtoto wa kike yamejumuisha washirika wa S4D wakiwemo TAMWA ZNZ. CYD, ZAFELA, na
GIZ.
No comments:
Post a Comment