Na, Fatma Rajab
Meneja msaidizi wa Hoteli ya maru maru Philip Mwakimu amesema wameanza na shughuli ya uandaaji wa keki ya krismasi ambapo ni desturi yao kila ifikapo mwezi mmoja kabla ya kufika krismasi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maandalizi ya keki ya kirsimas katika hotel ya Marumaru iliyopo mji mkongwe wilaya ya mjini.
Amesema dhamira kuu ya kufanya sherehe hizo ni kuendeleza utamaduni walio jiwekea kila mwisho wa mwaka pamoja na kujitangaza kibiashara na mataifa mbali mbali, pamoja na kuwa kivutio kwa watalii wanaotembelea nchini.
Nae mpishi mtendaji wa hoteli hiyo SK FIRDOUSH amesema katika mchanganyiko wa keki hiyo kunavitu mbali mbali ambavyo vinachanganywa katika keki hiyo ikiwemo tundadamu,papai,korosho,zabibu,cheza, na matunda mengine, ili kutengeneza kuwa na ladha nzuri.
kwa upande wake mpishi msaidizi chef Mohammed Abdallah amesema keki hio ina uzito wa kilo 75 na inatosheleza zaidi ya watu mia
Thank you for sharing
ReplyDelete