Na. Fatma Rajab
Wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi imewataka watembezaji wageni na walinzi katika maeneo ya hifadhi kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuweza kuepusha matukio kyasiyofaa.
Hayo yameelezwa na katibu mkuu wizara ya uchumi wa buluu Mh. Hamad Bakar Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa kutano wa zura wilaya ya mjini unguja.
amesema wizara inakemea vikali tukio la kutotii amri kwa mmoja ya watembezaji wa wageni katika hifadhi ya mnemba (MIMCA) pamoja na sitofahamu iliyojitokeza baina ya walinzi na watembezaji wageni siku ya jumatano ya tarehe 20.11.2024.
Amesema tukio hilo linakwenda kinyume na sheria na taratibu za kusimamia hifadhi zetu, wizara kwa kushirikiana na kamisheni ya utalii KMKM pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hatua kali zitachukuliwa kwa atakaebainika kwenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.
Hata hivyo wizara kupitia idara ya uhifadhi wa bahari inaendelea kutoa mafunzo kwa walinzi wake na elimu kwa jamii juu ya kufahamu namna bora ya kuendesha shughuli za utalii katika maeneo ya bahari zanzibar
No comments:
Post a Comment