Na, Fatma Rajab.
Chama
cha waandishi wa Habari wanawake Zanzibar TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau
wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Taasisi ya ZACCA ppamoja na Afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar,
imeandaa mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabianchi Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 20 hadi 22
katika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa kamati ya Jukwaa la mabadiliko ya
tabianchi Zanzibar.(ZANCCC) Mahfudh Shaban Haji, amesema lengo la mkutano huo
ni kujenga uwezo, uelewa na hamasa kwa asasi za kiraia, wanajamii na idara za
Serikali kufahamu dhana nzima ya mabadiliko ya tabianchi na uhimili wake.
Aidha Shaaban ameeleza kuwa katika mkutano huo
mikakati mbali mbali ya kitaifa na kimataifa, kama vile mkakati wa mabadiliko
ya tabia nchi wa mwaka 2024, sera na mkakati wa uchumi wa buluu, uwajibikaji na
matumizi sahihi ya rasilimali za nchi.
Aliongeza
kusema kuwa mipango ya nishati safi na mpango wa kitaifa wa maendeleo ya
Zanzibar (ZADEP) wa mwaka 2021-2026, na Dira ya Maendeleo ya 2050 inakwenda
sambamba na mipango ya kimataifa ya Maendeleo endelevu.
‘Tunafahamu
kwa kina kuwa mabadiliko ya Tabianchi ni suala mtambuka mkutano utaainisha
lengo hili la maendeleo endelevu la 23 na malengo mengine 16 yaliyokusudiwa kupitia vipindi na mada mbali mbali’’
ameongeza Mahfudh.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ Dkt Mzuri Issa amewataka waandishi wa Habari
kuandika habari zinazoibua changamoto za mabadiliko ya tabianchi ili ziweze
kuwafikia walengwa na kufanyiwa kazi.
‘’waandishi wahabari tumieni kalamu zenu kuyaibua
na kuyafanyia uchambuzi masuala ya mabadiliko ya tabianchi aliongeza kusema.Dkt
Mzuri.
Mwakilishi wa Taasisi ya kukabiliana na
manadiliko ya tabianchi ZACCA Ngwali O. Ngwali amesema Ukataji wa mikoko
unachochea zaidi mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya fukwe za Bahari
ambapo katika maeneo ya Mkokotoni,fungurefu na Donge yameathirika kwa kiasi
kikubwa.
Aidha
ameitaka jamii kuyalinda mazingira ili kuhakikisha Zanzibar ya kijani
inapatikana.
Jumla
ya wadau 35 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wenye kauli mbiu “ imarisha
uhimili wa mabadiliko ya tabianchi Zanzibar “
No comments:
Post a Comment