Mhe, Hemed Ashiriki siku ya Maadhimisho Siku ya Maadili

 

Na, Mwandishi wetu



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binaadamu Zanzibar  yana lengo ya kuwaongezea uwelewa viongozi wa umma na wananchi kuhusu umuhimu wa maadili, Utawala wa Sheria, haki na usawa, uadilifu na uwajibikaji pamoja na kuzuia rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma.

Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binaadamu Zanzibar yaliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.

 Amesema kila Taasisi na mwanachama kwa nafasi yake anapaswa kuhakikisha anatekeleza misingi ya utawala bora ili kuimarisha uadilifu, haki za Binaadamu na kuzuia rushwa ili Serikali iweze kufikia malengo yake ya kuwapatia maendeleo wananchi wake.

Makamu wa Pili wa Rais amesema Taasisi zinazosimamia Utawala bora ikiwemo Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora zimepiga hatua na zinaendelea kupata mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kudhibiti mianya ya rushwa, upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kuhakikisha kwamba fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha za matumizi ya kawaida kwa kila mwezi zinazopelekwa katika kila Wizara, Idara na Taasisi zinatumika kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais amesema kuongezeka kwa idadi ya hati safi za ukaguzi ni uthibitisho tosha  unaoonesha kuwepo kwa uwajibikaji katika usimamizi na matumizi ya rasilimali za umma uliopelekea kuimarika kwa huduma bora na ustawi wa jamii ikiwemo Miundombinu, Elimu, huduma za Afya, Umeme na Maji.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewakumbusha viongozi wote kufanya kazi zao kwa kufuata sheria na miongozo ya kazi zao na kutoa maelekezo kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushirikiana na Mamlaka nyengine husika kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu zinazostahiki kwa  mujibu wa sheria viongozi wote wanaolalamikiwa kuvunja maadili katika nchi.

Nae waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Mwalimu Haroun Ali Suleiman amesema ni jukumu la Viongozi na watumishi wa Umma kuwa na Uzalendo, Uwajibikaji, Uwazi na Uadilifu ambavyo ndio vigezo  na mihimili ya Utawala bora wenye kufuata sheria na maadili.

 

 

 Mhe. Harun amesema katika kuhakikisha elimu ya Maadili na Utawala bora inawafiki viongozi, watumishi wa umma na wananchi wote, Wizara yake imeanzisha Online TV ambayo inalenga kufikisha Taaluma kwa kuandaa Vipindi vitakavyoonesha utendaji kazi wa Wizara na Taasisi  zote za Serikali na Binafsi ili kutanua wigo na uwelewa mpana wa Haki za Binaadamu nchini.

 

Akiwasilisha maada katika maadhimisho hayo  juu ya umuhimu wa usimamizi wa Rasilimali za umma na Mapambano dhidi ya Rushwa katika kuimarisha Utawala Bora Mhe. Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim ameelezea makosa mbali mbali ya kisheria ambayo viongozi na watumishi wa umma wanatakiwa kujiepusha nayo ikiwemo kutoa na kupokea rushwa, usimamizi na matumizi mabaya ya rasilimali za Umma  pamoja na matumizi mabaya ya madaraka  .

Jaji Ibrahim amesema Viongozi na watumishi wa Umma ni vyema kujiepusha na yale yote yaliyotajwa katika kifungu cha 18, Sheria namba 4 ya mwaka 2015, Sheria ya maadili ya Viongozi wa umma Zanzibar ili kuendelea kuwa na viongozi bora wenye kufuata sheria, miongozo na Maadili ya Viongoziwa Umma kwa maslahi mapana ya nchi.

Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binaadamu hufanyika kila ifikapo Disemba 10 ya kila mwaka ambayo yanaenda sambamba na siku ya mapambano dhidi ya rushwa ambayo hufanyika kila ifikapo Disemba 9 ya kila mwaka ambapo kwa upande wa Zanzibar maadhimisho hayo hufanywa sambamba Disemba 10 ambapo hubeba maudhui yenye mnasaba na siku hizo.s

 

 

 

 


Watembezaji watalii watakiwa kufuata Sheria

 



Na. Fatma Rajab

Wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi imewataka watembezaji wageni na walinzi katika maeneo ya hifadhi  kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuweza kuepusha matukio kyasiyofaa.

Hayo yameelezwa na katibu mkuu wizara ya uchumi wa buluu  Mh. Hamad Bakar Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa kutano wa zura wilaya ya mjini unguja.

amesema wizara inakemea vikali tukio la kutotii amri kwa mmoja ya watembezaji wa wageni katika hifadhi ya mnemba  (MIMCA) pamoja na sitofahamu iliyojitokeza baina ya walinzi na watembezaji wageni siku ya jumatano ya tarehe 20.11.2024.


Amesema tukio hilo linakwenda kinyume na sheria na taratibu za kusimamia hifadhi zetu, wizara kwa kushirikiana na kamisheni ya utalii KMKM pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hatua kali zitachukuliwa kwa atakaebainika kwenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.


Hata hivyo wizara kupitia idara ya uhifadhi wa bahari inaendelea kutoa mafunzo kwa walinzi wake na elimu kwa jamii juu ya  kufahamu namna bora ya kuendesha  shughuli za utalii katika maeneo ya bahari zanzibar

Maru Maru Hotel kuanza maandlizi ya Kirismas

 

                 Na, Fatma Rajab




Meneja msaidizi wa Hoteli ya  maru maru Philip Mwakimu  amesema wameanza na shughuli ya uandaaji wa keki ya krismasi ambapo ni desturi yao kila ifikapo mwezi mmoja kabla ya kufika krismasi.

Ameyasema hayo wakati  akizungumza na waandishi wa habari katika maandalizi ya keki ya kirsimas katika hotel ya Marumaru iliyopo mji mkongwe wilaya ya mjini.

 Amesema dhamira kuu ya kufanya sherehe hizo ni kuendeleza utamaduni walio jiwekea kila mwisho wa mwaka pamoja na kujitangaza  kibiashara na mataifa mbali mbali, pamoja na kuwa kivutio kwa watalii wanaotembelea nchini. 

 Nae mpishi mtendaji wa hoteli hiyo SK FIRDOUSH amesema katika mchanganyiko wa keki hiyo kunavitu mbali mbali ambavyo vinachanganywa katika keki hiyo ikiwemo tundadamu,papai,korosho,zabibu,cheza, na matunda mengine, ili kutengeneza kuwa na ladha nzuri.

kwa upande wake  mpishi msaidizi chef  Mohammed Abdallah amesema  keki hio  ina uzito wa kilo 75 na inatosheleza zaidi ya watu mia 


JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA MALEZI YA WATOTO

 

Na,Fatam Rajab



Jamii imetakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa  katika kuwalea watoto  katika maadili mema yenye kupwekesha Mwenyezi Mungu.

Hayo yameelezwa nakatibu wa kamati ya maadili kupitia baraza na Taasisi za kiislamu Zanzibar Abdalla Mnubi Abas ambae ni katibu wa kamati ya maadili kupitia Jumuiya ya maimamu Zanzibar wakati alipokuwa katika muhadhara wa kujadili suala zima la maadili kwa watoto katika kijiji cha banda kuu Nungwi Zanzibar.

Amesema vyuo vya madrasa vina  umuhimu mkubwa katika jamii na ni njia moja  ya watoto kukuwa katika maadili  mema na sehemu pekee ya kurudisha maadili katika jamii ni vyuo vya Qurani ambayo  hufundisha  tabia njema na kuacha tabia mbaya zisizokuwa na maadili

Aidha amesema"kutokana na uvamizi uiliopo katika kijiji cha Nungwi kuwepo kwa mahoteli na wageni mbali mbali ambao wanatoka ndani ya nchi na nje ya nchi kutofuata maadili na kuvaa vivazi ambavyo havifai.

Aidha,amewataka wazazi na walezi kuiga malezi ambayo waliolelewa na wazee wa zamani na kuishi kirafiki na watoto wao ili kugundua changamoto wanazo kumbana nazo.

Kwa upande wake sheha wa shehia ya bandaa kuu Nungwi Haji Khamis Haji  amesma tatizo la maadili limekuwa kubwa katika jamii na linatokana na changamoto mbali mbali ikiwemo mazizngira, wigo, na uingiaji wa wageni kiholela.

  Amesema mikakati mabli mbali ambayo imechukuliwa katika kijiji hicho ikiwemo ya kiwekwa mihadhra yenye kuelimisha watu katika suala zima la maadili, pia amesisitiza wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao na kuwap elimu kuhisiana na masula ya kumcha Allah ili waweze kuepukana na vitendo viovu.

Akitoa wito kwa wageni Ndg Haji Khamis Haji amesema "wageni wanatakiwa kungalia jamii inaishi vipi ili kuepusha upotevu wa maadaili endapo watafika katika jamii na wanatakiwa kuzingatia sharia za sehemu husika.

Hata hivyo wazazi na walezi wa kijiji hicho wamaitaka  jumuiya  ya maimu kuwasaidia katika malezi na kukza maadili ya jamii ili kuwa na kazazi chema chenye kufuata maadili mema .




 Na Fatma Rajab



Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia  Wazee, na Watoto Zanzibar, Mhe. Anna Athanas Paul amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto inamuonesha kuwa na haki ya kucheza Michezo ya aina yoyote hivyo ameitaka Jamii kuunga mkono juhudi za Watoto katika harakati za kujijengea uwezo kupitia michezo.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia Michezo ya Watoto katika Viwanja vya Mou Tes Tung amesema, Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar wataendelea kuunga mkono shughuli za michezo kwa Watoto na kuwalinda katika nyanja zote za maisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya za Michezo zilizochini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hashim Pondeza amesema, Wanawake wanapaswa kushiriki katika Michezo kwa misingi ya mila na desturi, hivyo ameitaka Jamii kuendelea kuwahamasisha Watoto kushiriki katika Michezo mbalimbali ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uelewa na kujiamini katika harakati zao za kila siku.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya za Michezo zilizochini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hashim Pondeza amesema, Wanawake wanapaswa kushiriki katika Michezo kwa misingi ya mila na desturi, hivyo ameitaka Jamii kuendelea kuwahamasisha Watoto kushiriki katika Michezo mbalimbali ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uelewa na kujiamini katika harakati zao za kila siku.

Kwa upande wake Afisa Programu kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA ZNZ Asia Hakim Makame amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuelimisha jamii, umuhimu wa mtoto wa kike kushiriki katika michezo na kufikia ndoto zao.

Maadhimisho hayoya siku ya mtoto wa kike yamejumuisha washirika wa S4D wakiwemo TAMWA ZNZ. CYD, ZAFELA, na GIZ.

Mikakati kukabiliana na Tabia ya Nchi yaanza Kuchukuliwa

 

Na, Fatma Rajab.



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimekuwa zikichukuwa hatua mbali mbali  kuweza  kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuingiza mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye mipango ya Taifa ya maendeleo kama vile  dira ya Taifa ya maendeleo ya zanzibar ya mwaka 2025 na mpango wa maeneleo ya zanzibar wa 2021 2026..

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman wakati alipohudhuria mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya  tabia ya nchi uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil  kikwajuni Zanzibar,

 Amesema serikali imetaarisha mkakati wa mabadiliko ya Tabia ya nchi wa zanzibar wa mwaka 2014 ambao umeeleza vipaumbele  na hatua zinazofaa kuchukuliwa na kukabiliana na mabadiliko hayo kuwepo kwa hatua mbali mbali za  kupanda miti ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na miti ya mikoko, mitandaa  katika maeneo ya fukwe ili kupunguza kasi ya uingiaji wa maji ya bahari katika maeneo ya kilimo kwa lengo la kuwafanya wananchi wetu kuendelea kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kilimo na kiuchumi"


Aidha amesema katika kipindi cha miaka 30 iliyopita wastani wa kiwango cha joto kilipanda ongezeko kubwa la kiwango cha juu cha joto kufikia nyuzi joto 39"  hivi  karibuni imeshuhudia mvua zisizotambulika wakati mwengine zinanyesha kubwa na kupelekea mafuriko wakati mwengine zinanyesha kinyume na wakati tusioutarajia haya yote ni yanatokana na athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi,.

Aliongeza kusema  kuwa maeneo ya ukanda wa pwani yaliyochini ya muinuko wa mita 5 yapo kwenye  tishio la kuathirika na kupanda kwa kina cha bahari na maeneo hayo kwa unguja yanajumala ya kilomita  za mraba 328 na kwa kisiwa cha pemba yana kilimita za mraba 286.

Kwa  mujibua  wa taarifa zilizokusanywa na na afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais mwaka 2012 Zanzibar ina jumala ya maeneo 148 yakiwemo pemba 123 na Unguja  25 yanaingia maji ya chumvi na zaid yakitumiwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi, kilimo kijamii lakini kutokana na kuingia maji ya chumvi yanayosababisha kupanda kwa kina cha bahari wananchi wa maeneo hayo sasa hawawezi tena kuendelea na shughuli zozote katika maeneo hayo

Aikizitaja sekata za kiuchumi zilizo athirika zaidi na mabadiliko ya Tabia ya nchi Mhe Harusi amesema"sekata za kiuchumi zilizoonekana kuathirika zaidi hapa  Zanzibar ni uvuvi wa ukanda wa pwani, ukulima wa mwani ,kilimo ,utalii,maji makaazi na miundombinu".

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Zanzibar Climate Change alliance ZACCA ambae pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabia ya nchi  Mahfoudh Shaaban amesema kuna tathimini ambazo wamezifanya wao kama zacca kwa kushirikiana na wadau wengine ni kuweza kuchunguza uwelewa na ufahamu lakini pia ni kutaka kujua ni naman gani ya wadau mbali mbali kuanzia serikali mpaka wadau wa asasi za kiraia wanaweza kuhimili athari za mabadiliko ya tabia y nchi.

Hatahivyo amesema kuwa tathimin hiyo imeonesha kuna uwazi mkubwa wa watu kuelewa masuala hayo hivyo mkutana huo una lengo la kujenga uwelewa wa kuendeleza na kuimarisha nguvu za pamoja  katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi hapa Zanzibar.

 


Baraza la sanaa, sensa ya filamu Zanzibar lapiga marufuku Baa zote ambazo hazina Sound Proof

 


Na, Fatma Rajab


Baraza la sanaa, sensa ya filamu na utamaduni, (BASSFU) limezuia upigwaji wa mzuki katika maeneo ya baa zote ndani ya           Zanzibar ambazo hazina maeneo maalum ya kuzuia sauti (soundproof) ili kuepusha usumbufu  unaosababishwa na sauti ya muziki kwa watu mbali mbali ikiwemo wanaofanya ibada, watalii, wagonjwa, wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na katibu mtendaji baraza la sanaa,  sensa ya filamu na utamaduni Chuom Juma Chuom wakati alipokuw akizungumza na waabdishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa studio ZBC  raha leo zanzibar

Amesema "uamuzi haukuja kwamba tumeamua kuzuia sanaa bali lengo la uamuzi huu ni kutaka jamii ibaki salama dhidi ya maudhi yanayotokana na sauti za upigaji wa mziki katika maeneo ya mabaa ambapo watu wa ibada wwfanya biashara mbali mbali ikiwemo biashara ya utalii, wanafunzi ambao wapo katika mskuli mbali mbali lakini pia na jamii kwa ujumla imekua ikiathirika kutokana na upigaji wa mziki kiholela".

Lengo jengine la uamuzi huo ni kutaka kuweka ustawi mzuri wa jamii amesema" hatuna dhamira mbaya ya kukwaza shughuli za sanaa na burudani tunataka sana, tunapenda sana serikali yetu inayoongozwa na raisi dkt hussein ali mwinyi na waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo ni wapenzi wa sanaa na burudani lakini kwa vile kuna wananchi wanaoongoza tunachotaka kwa pamoja ni kutoa fursa kwa sanaa na burudani yenye kufuata maadili mila desturi na ustawi wa kijamii".

Aidha amesema baraza la sanaa limejipnga kwa kushirikiana na vyombo mbali mbali vya serikali ikiwemo jeshi la polisi, afisi za wakuu wa wilaya, masheha ,wakurugenzi wa manispaa pamoja na halmashauri kuhakikisha wanadhibiti baa ambazo zinapiga mziki usiozingatia taratibu na sheria zilizopangwa ikiwemo za kuwepo maeneo maalum ya kudhibiti sauti.

Hata hivyo amesema baraza la sanaa halitatoa leseni katika maeneo ya mabaa ambayo hayana maeneo maalum ya kudhibiti sauti (soundproof)"kwa maeneo ambayo  tayari yameshahenga maeneo ya soundproof tutaendelea kutoa leseni katika maeneo hayo lakini pia tutaendelea kuyasimamia kufanya shughuli za sanaa na  burudani kwa misingi ya taratibu, sheria kanuni na miongozo mbali mbali ambayo ipo na tunaendelae kuwapatia".

Hiyvo baraza la baraza linaendelea kufanya ziara za ukaguzi katika maeneo yote ya burudani kwa lengo la kudhibiti athari zinazotokana na kelele za muziki kwa jamii," sisi baraza la sanaa kwa kushirikiana na mamlaka ambazo tumezitaja kesho tutafanya operesheni kali ya kudhibiti na kuchkukua hatua kali kwa taasisi ama mtu yoyote ataekwenda kunyume na taarifa hii".


ZSTC yaridhiishwa na Chuo cha Mafunzo Katika Uimarishaji wa Zao la Karafuu

  Na. Mwandishi Wetu. Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Nd. Soud Said Ali amesema Shirika la Biashara Z...