JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA MALEZI YA WATOTO

 

Na,Fatam Rajab



Jamii imetakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa  katika kuwalea watoto  katika maadili mema yenye kupwekesha Mwenyezi Mungu.

Hayo yameelezwa nakatibu wa kamati ya maadili kupitia baraza na Taasisi za kiislamu Zanzibar Abdalla Mnubi Abas ambae ni katibu wa kamati ya maadili kupitia Jumuiya ya maimamu Zanzibar wakati alipokuwa katika muhadhara wa kujadili suala zima la maadili kwa watoto katika kijiji cha banda kuu Nungwi Zanzibar.

Amesema vyuo vya madrasa vina  umuhimu mkubwa katika jamii na ni njia moja  ya watoto kukuwa katika maadili  mema na sehemu pekee ya kurudisha maadili katika jamii ni vyuo vya Qurani ambayo  hufundisha  tabia njema na kuacha tabia mbaya zisizokuwa na maadili

Aidha amesema"kutokana na uvamizi uiliopo katika kijiji cha Nungwi kuwepo kwa mahoteli na wageni mbali mbali ambao wanatoka ndani ya nchi na nje ya nchi kutofuata maadili na kuvaa vivazi ambavyo havifai.

Aidha,amewataka wazazi na walezi kuiga malezi ambayo waliolelewa na wazee wa zamani na kuishi kirafiki na watoto wao ili kugundua changamoto wanazo kumbana nazo.

Kwa upande wake sheha wa shehia ya bandaa kuu Nungwi Haji Khamis Haji  amesma tatizo la maadili limekuwa kubwa katika jamii na linatokana na changamoto mbali mbali ikiwemo mazizngira, wigo, na uingiaji wa wageni kiholela.

  Amesema mikakati mabli mbali ambayo imechukuliwa katika kijiji hicho ikiwemo ya kiwekwa mihadhra yenye kuelimisha watu katika suala zima la maadili, pia amesisitiza wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao na kuwap elimu kuhisiana na masula ya kumcha Allah ili waweze kuepukana na vitendo viovu.

Akitoa wito kwa wageni Ndg Haji Khamis Haji amesema "wageni wanatakiwa kungalia jamii inaishi vipi ili kuepusha upotevu wa maadaili endapo watafika katika jamii na wanatakiwa kuzingatia sharia za sehemu husika.

Hata hivyo wazazi na walezi wa kijiji hicho wamaitaka  jumuiya  ya maimu kuwasaidia katika malezi na kukza maadili ya jamii ili kuwa na kazazi chema chenye kufuata maadili mema .




 Na Fatma Rajab



Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia  Wazee, na Watoto Zanzibar, Mhe. Anna Athanas Paul amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto inamuonesha kuwa na haki ya kucheza Michezo ya aina yoyote hivyo ameitaka Jamii kuunga mkono juhudi za Watoto katika harakati za kujijengea uwezo kupitia michezo.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia Michezo ya Watoto katika Viwanja vya Mou Tes Tung amesema, Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar wataendelea kuunga mkono shughuli za michezo kwa Watoto na kuwalinda katika nyanja zote za maisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya za Michezo zilizochini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hashim Pondeza amesema, Wanawake wanapaswa kushiriki katika Michezo kwa misingi ya mila na desturi, hivyo ameitaka Jamii kuendelea kuwahamasisha Watoto kushiriki katika Michezo mbalimbali ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uelewa na kujiamini katika harakati zao za kila siku.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya za Michezo zilizochini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hashim Pondeza amesema, Wanawake wanapaswa kushiriki katika Michezo kwa misingi ya mila na desturi, hivyo ameitaka Jamii kuendelea kuwahamasisha Watoto kushiriki katika Michezo mbalimbali ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uelewa na kujiamini katika harakati zao za kila siku.

Kwa upande wake Afisa Programu kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA ZNZ Asia Hakim Makame amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuelimisha jamii, umuhimu wa mtoto wa kike kushiriki katika michezo na kufikia ndoto zao.

Maadhimisho hayoya siku ya mtoto wa kike yamejumuisha washirika wa S4D wakiwemo TAMWA ZNZ. CYD, ZAFELA, na GIZ.

Mikakati kukabiliana na Tabia ya Nchi yaanza Kuchukuliwa

 

Na, Fatma Rajab.



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimekuwa zikichukuwa hatua mbali mbali  kuweza  kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuingiza mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye mipango ya Taifa ya maendeleo kama vile  dira ya Taifa ya maendeleo ya zanzibar ya mwaka 2025 na mpango wa maeneleo ya zanzibar wa 2021 2026..

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman wakati alipohudhuria mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya  tabia ya nchi uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil  kikwajuni Zanzibar,

 Amesema serikali imetaarisha mkakati wa mabadiliko ya Tabia ya nchi wa zanzibar wa mwaka 2014 ambao umeeleza vipaumbele  na hatua zinazofaa kuchukuliwa na kukabiliana na mabadiliko hayo kuwepo kwa hatua mbali mbali za  kupanda miti ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na miti ya mikoko, mitandaa  katika maeneo ya fukwe ili kupunguza kasi ya uingiaji wa maji ya bahari katika maeneo ya kilimo kwa lengo la kuwafanya wananchi wetu kuendelea kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kilimo na kiuchumi"


Aidha amesema katika kipindi cha miaka 30 iliyopita wastani wa kiwango cha joto kilipanda ongezeko kubwa la kiwango cha juu cha joto kufikia nyuzi joto 39"  hivi  karibuni imeshuhudia mvua zisizotambulika wakati mwengine zinanyesha kubwa na kupelekea mafuriko wakati mwengine zinanyesha kinyume na wakati tusioutarajia haya yote ni yanatokana na athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi,.

Aliongeza kusema  kuwa maeneo ya ukanda wa pwani yaliyochini ya muinuko wa mita 5 yapo kwenye  tishio la kuathirika na kupanda kwa kina cha bahari na maeneo hayo kwa unguja yanajumala ya kilomita  za mraba 328 na kwa kisiwa cha pemba yana kilimita za mraba 286.

Kwa  mujibua  wa taarifa zilizokusanywa na na afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais mwaka 2012 Zanzibar ina jumala ya maeneo 148 yakiwemo pemba 123 na Unguja  25 yanaingia maji ya chumvi na zaid yakitumiwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi, kilimo kijamii lakini kutokana na kuingia maji ya chumvi yanayosababisha kupanda kwa kina cha bahari wananchi wa maeneo hayo sasa hawawezi tena kuendelea na shughuli zozote katika maeneo hayo

Aikizitaja sekata za kiuchumi zilizo athirika zaidi na mabadiliko ya Tabia ya nchi Mhe Harusi amesema"sekata za kiuchumi zilizoonekana kuathirika zaidi hapa  Zanzibar ni uvuvi wa ukanda wa pwani, ukulima wa mwani ,kilimo ,utalii,maji makaazi na miundombinu".

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Zanzibar Climate Change alliance ZACCA ambae pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabia ya nchi  Mahfoudh Shaaban amesema kuna tathimini ambazo wamezifanya wao kama zacca kwa kushirikiana na wadau wengine ni kuweza kuchunguza uwelewa na ufahamu lakini pia ni kutaka kujua ni naman gani ya wadau mbali mbali kuanzia serikali mpaka wadau wa asasi za kiraia wanaweza kuhimili athari za mabadiliko ya tabia y nchi.

Hatahivyo amesema kuwa tathimin hiyo imeonesha kuna uwazi mkubwa wa watu kuelewa masuala hayo hivyo mkutana huo una lengo la kujenga uwelewa wa kuendeleza na kuimarisha nguvu za pamoja  katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi hapa Zanzibar.

 


Baraza la sanaa, sensa ya filamu Zanzibar lapiga marufuku Baa zote ambazo hazina Sound Proof

 


Na, Fatma Rajab


Baraza la sanaa, sensa ya filamu na utamaduni, (BASSFU) limezuia upigwaji wa mzuki katika maeneo ya baa zote ndani ya           Zanzibar ambazo hazina maeneo maalum ya kuzuia sauti (soundproof) ili kuepusha usumbufu  unaosababishwa na sauti ya muziki kwa watu mbali mbali ikiwemo wanaofanya ibada, watalii, wagonjwa, wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na katibu mtendaji baraza la sanaa,  sensa ya filamu na utamaduni Chuom Juma Chuom wakati alipokuw akizungumza na waabdishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa studio ZBC  raha leo zanzibar

Amesema "uamuzi haukuja kwamba tumeamua kuzuia sanaa bali lengo la uamuzi huu ni kutaka jamii ibaki salama dhidi ya maudhi yanayotokana na sauti za upigaji wa mziki katika maeneo ya mabaa ambapo watu wa ibada wwfanya biashara mbali mbali ikiwemo biashara ya utalii, wanafunzi ambao wapo katika mskuli mbali mbali lakini pia na jamii kwa ujumla imekua ikiathirika kutokana na upigaji wa mziki kiholela".

Lengo jengine la uamuzi huo ni kutaka kuweka ustawi mzuri wa jamii amesema" hatuna dhamira mbaya ya kukwaza shughuli za sanaa na burudani tunataka sana, tunapenda sana serikali yetu inayoongozwa na raisi dkt hussein ali mwinyi na waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo ni wapenzi wa sanaa na burudani lakini kwa vile kuna wananchi wanaoongoza tunachotaka kwa pamoja ni kutoa fursa kwa sanaa na burudani yenye kufuata maadili mila desturi na ustawi wa kijamii".

Aidha amesema baraza la sanaa limejipnga kwa kushirikiana na vyombo mbali mbali vya serikali ikiwemo jeshi la polisi, afisi za wakuu wa wilaya, masheha ,wakurugenzi wa manispaa pamoja na halmashauri kuhakikisha wanadhibiti baa ambazo zinapiga mziki usiozingatia taratibu na sheria zilizopangwa ikiwemo za kuwepo maeneo maalum ya kudhibiti sauti.

Hata hivyo amesema baraza la sanaa halitatoa leseni katika maeneo ya mabaa ambayo hayana maeneo maalum ya kudhibiti sauti (soundproof)"kwa maeneo ambayo  tayari yameshahenga maeneo ya soundproof tutaendelea kutoa leseni katika maeneo hayo lakini pia tutaendelea kuyasimamia kufanya shughuli za sanaa na  burudani kwa misingi ya taratibu, sheria kanuni na miongozo mbali mbali ambayo ipo na tunaendelae kuwapatia".

Hiyvo baraza la baraza linaendelea kufanya ziara za ukaguzi katika maeneo yote ya burudani kwa lengo la kudhibiti athari zinazotokana na kelele za muziki kwa jamii," sisi baraza la sanaa kwa kushirikiana na mamlaka ambazo tumezitaja kesho tutafanya operesheni kali ya kudhibiti na kuchkukua hatua kali kwa taasisi ama mtu yoyote ataekwenda kunyume na taarifa hii".


TAMWA ZNZ Kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Wa Rais Kupambana na Tabianchi

 

Na, Fatma Rajab.





Chama cha waandishi wa Habari wanawake Zanzibar TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Taasisi ya  ZACCA ppamoja na  Afisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar, imeandaa mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabianchi Zanzibar,  unaotarajiwa kufanyika Oktoba 20 hadi 22 katika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa kamati ya Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.(ZANCCC) Mahfudh Shaban Haji, amesema lengo la mkutano huo ni kujenga uwezo, uelewa na hamasa kwa asasi za kiraia, wanajamii na idara za Serikali kufahamu dhana nzima ya mabadiliko ya tabianchi na uhimili wake.

 Aidha Shaaban ameeleza kuwa katika mkutano huo mikakati mbali mbali ya kitaifa na kimataifa, kama vile mkakati wa mabadiliko ya tabia nchi wa mwaka 2024, sera na mkakati wa uchumi wa buluu, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi.

Aliongeza kusema kuwa mipango ya nishati safi na mpango wa kitaifa wa maendeleo ya Zanzibar (ZADEP) wa mwaka 2021-2026, na Dira ya Maendeleo ya 2050 inakwenda sambamba na mipango ya kimataifa ya Maendeleo endelevu.

‘Tunafahamu kwa kina kuwa mabadiliko ya Tabianchi ni suala mtambuka mkutano utaainisha lengo hili la maendeleo endelevu la 23 na malengo mengine 16 yaliyokusudiwa  kupitia vipindi na mada mbali mbali’’ ameongeza  Mahfudh.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ Dkt Mzuri Issa amewataka waandishi wa Habari kuandika habari zinazoibua changamoto za mabadiliko ya tabianchi ili ziweze kuwafikia walengwa na kufanyiwa kazi.

 ‘’waandishi wahabari tumieni kalamu zenu kuyaibua na kuyafanyia uchambuzi masuala ya mabadiliko ya tabianchi aliongeza kusema.Dkt Mzuri.

 Mwakilishi wa Taasisi ya kukabiliana na manadiliko ya tabianchi ZACCA Ngwali O. Ngwali amesema Ukataji wa mikoko unachochea zaidi mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya fukwe za Bahari ambapo katika maeneo ya Mkokotoni,fungurefu na Donge yameathirika kwa kiasi kikubwa.

Aidha ameitaka jamii kuyalinda mazingira ili kuhakikisha Zanzibar ya kijani inapatikana.

Jumla ya wadau 35 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wenye kauli mbiu “ imarisha uhimili wa mabadiliko ya tabianchi Zanzibar “

 


Ujio wa Mufti ISMAIL BIN MUSSA MENKI ZANZIBAR KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

 


Na.Fatma Rajab



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Ujio wa Mufti ISMAIL BIN MUSSA MENKI kutoka nchini  Zimbabwe umetoa fursa kwa Zanzibar kujitangaza zaidi kiutalii kupitia Utalii wa Maadili yani (HALAL TOURISM) uliojikita zaidi katika sheria na misingi ya Uislamu.

Ameyasema hayo katika hafla ya JUKWAA la UWEKEZAJI wa Utalii halali (HALAL TOURISM) lililofanyika katika Viwanja vya  Hotel ya Verde Mtoni jijini Zanzibar.

Amesema uwepo wa Mufti Menki nchini umeitangaza Zanzibar kiutalii na kupata fursa ya kujifunza mambo mbali mbali kupitia Jukwaa la Utalii wa maadili lililotoa fursa kwa Mufti huyo na ujumbe wake aliokuja nao katika kuukumbusha umma umuhimu wa mikusanyiko ya dini na kuwa tayari kujitoa kwa ajili ya Allah.

Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu mbali mbali ikiwemo ya barabara, Viwanja vya ndege na Bandari ambavyo vinachochea ukuwaji wa sekta ya Utalii nchini sambamba na kuviboresha vivutio vya utalii ili kuendelea kujitangaza kiutalii hasa katika maeneo ya kihistoria, kutangaza mila, silka na tamaduni njema zinazofuata mwenendo mzima wa kiislam ikiwemo Ibada, mavazi, ukarimu na ushirikiano katika jamii.

Aidha, Mhe.Hemed amefahamisha kuwa Serikali kupitia Kamisheni ya Utalii inaendelea kufanya mapitio ya mwisho ya Sera ya Utalii ya Zanzibar ya Mwaka 2017 kwa lengo la kuifanyia maboresho ikiwemo eneo la Utalii wa maadili kwa kuweka mikakati mbili mbali itakayosaidia kukuza utalii wa kiislam hapa Zanzibar.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuahidi Mufti Menki na ujumbe wake kuwa Serikali na waislamu kwa ujumla watayafanyia kazi yale yote waliyojifunza kutoka kwako na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar kiutalii hasa katika Utalii wa maadili na kuwahamasisha wataalamu  mbali mbali wa Kiislamu kuja Zanzibar kufanya Tafiti za historia ya kiislam zitakazosaidia kuitangaza dini na  Zanzibar kwa ujumla.

Nae Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga ameishukuru Kampuni ya Light upon Light kwa kuamua kufanya Jukwaa la Utalii wa maadili Visiwani Zanzibar ambalo litasaidia katika kuitangaza Zanzibar kiutalii na kutanua wigo kwa wageni wengi zaidi kuitembelea Zanzibar.

Mhe. Soraga amesema Jukwaa la Utalii wa maadili ni muhimu katika maendelea ya Zanzibar na kila kilichojadiliwa katika Jukwaa hilo kinalenga katika kuiendeleza Zanzibar kiutalii na kuifanya kuwa Kituo kikubwa cha Utalii Barani Afrika, hivyo atahakikisha kuwa Wizara inachukua juhudi za maksudi kuviboresha vivutio vya utalii na kuanzisha vipya ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea.



Kwa upande wake Mufti ISMAIL BIN MUSSA MENKI kutoka nchini Zimbabwe ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wazanzibari kwa ujumla kwa mapokezi ya heshima, upendo na ukarimu walionaompatia yeye na ujumbe wake jambo linalompa faraja ya kuendelea kuitembelea tena Zanzibar na kuahidi kutangaza mazuri yote waliyojifunza Zanzibar .

Amesema kila binaadamu ana wajibu wa kuzitumia neema alizojaaliwa na Allah katika kuisimamia Dini ya kiislam na kuwa tayari kutoa neema hizo kwa ajili ya kuwasaidia wasio na uwezo na wenye mazingira magumu kwa kutambua hilo ndio lengo la kuletwa kwake Duniani kuja kumtumikia Allah (S.W).

Mufti Menki amesema miongoni mwa Ibada anazotakiwa kufanya muislamu ni kufanya kazi ya halali kwa kufuata misingi ya Dini ya kiislamu jambo litakalosaidia waislamu kuishi kwa upendo na kusaidiana pamoja na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

 

 


Serikali Kutoa Mafunzo kwa walimu wa SMZ

 

Na,  Mwandishi Wetu.




Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar itaendelea kuhakikisha walimu wanapata mafunzo wakiwa kazini yatakayowasaidia kuongeza ujuzi wa hali ya juu ambao utawasaidia katika kutekeleza mfumo mpya wa elimu.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Walimi Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema ni jambo la muhimu sana kufanyika kwa Maadhimisho ya siku ya walimu duniani yanayolenga kutathmini mafanikio na changamoto za walimu katika kufikia mapendekezo ya hadhi ya walimu yaliyowekwa na UNESCO na ILO yanayosisitiza Taaluma, mazingira bora, hadhi, heshima na maslahi ya walimu.

Mhe.Hemed amesema Serikali katika kulinda hadhi na maslahi ya walimu imeanzisha Tume ya Utumishi ya walimu ambayo madhumuni yake ni kusimamia ustawi na kuendeleza kutunza heshima ya walimu pamoja na kusimamia ujenzi wa makaazi ya walimu na dahalia za wanafunzi katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Serikali imekusudia kujenga chuo cha Uwalimu ambacho kitatumika kutoa mafunzo kwa walimu na kuwajengea uwezo unaoendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknoloji duniani ili waweze kufundisha kwa ufanisi zaidi.

Sambamba na hilo Makamu wa Pili wa Rais amewataka walimu kuitumia vyema fursa ya kukusanyika pamoja kwa kubadilishana uzoefu na maarifa na kuliwekea msisitizo suala la uwajibikaji kazini, maadili mema kwa walimu na wanafunzi na kukumbusha sifa za mwalimu bora hasa katika kipindi hiki ambacho Zanzibar inafanya maguzi makubwa ya Mfumo wa elimu.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza kuwa serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu na mafunzo ya amali itahakikisha inazitatua changamoto zote zinazowakabili walimu ikiwemo malimbikizo ya fedha za likizo na ufiwa.

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohamed Mussa amesema walimu wana jukumu la kujiongeza  kitaaluma na  kujiendeleza kielimu kwa walimu wa ngazi zote ili kuendana na mageuzi ya mfumo wa elimu ambao unatumia zaidi Teknolojia na kuwafanya walimu waendane na matakwa ya elimu duniani.

Mhe. Lela amesema kwa kuhakikisha sekta ya elimu inazidi kuimarika Wizara ya elimu imekuwa ikikutana na Uwongizi wa chama cha wafanyakazi na chama cha walimu ili kujadili maslahi na ustawi wa walimu na sekta ya elimu kwa ujumla.

Amesema kuna changamoto nyingi zimejitokeza baada ya ugatuzi ikiwemo posho na nauli za walimu jambo ambalo lipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake na kuwaahidi walimu kuwa Serikali kupitia Wizara ya elimu itahakikisha maslahi na haki za walimu zinapatikana kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar ( ZATU ) Mwalimu HAJI JUMA amesema siki ya walimu duniani inatoa fursa kwa walimu kutafakari mafanikio na changamoto katika sekta ya elimu hasa katika kuinua viwango vya elimu na ustawi bora wa walimu na wanafunzi nchini.

Mwalimu HAJI ameiomba Serikali kuangalia umuhimu wa kuwashirikisha walimu ipasavyo hasa katika ngazi za maamuzi ili kuzidi kuiimarisha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wote wa Zanzibar.

Amesema ili kuendelea kuboresha sekta ya elimu na mazingira ya utowaji wa elimu bora nchini jitihada za pamoja zinahitajika kati ya Serikali, walimu na wazazi ili kutoa matokeo chanya ya  ufaulu kwa wanafunzi wa Zanzibar.

 

 

 




TAMWA (ZNZ) ZAFELA Kushirikiana katika michezo kukuza ushiriki wa Mtoto wakike.

 


Na, Fatma Rajab


 Wadau wa michezo kwa maendeleo Zanzibar ikiwemo Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania, (TAMWA ZNZ), Chama Cha wanasheria wanawake ZAFELA, Ktuo cha Mijadala kwa Vijana (CYD) pamoja na Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ) wameandaa shughuli mbali mbali za Michezo kwa maendeleo yenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika michezo na kujikinga na udhalilishaji wa kijinsia kijinsia katika 

Hayo yameelezwa na Afisa programu kutoka TAMWA (ZNZ) Khairat  Haji  Ali wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika ukumbi wa mkutano wa viwanja vya mau  Zanzibar.

Amesema maadhimisho hayo yana lengo la kuimarisha watoto wa kike kushiriki katika michezo pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambayo kwa asilimia kubwa   vinawakumba watoto wa kike.katika michezo


 


Aidha amesema, kuelekea maadhimisho hayo wameandaa ziara ya kutembelea Skuli mbali mbali na kuendesha shughuli za michezo kwa maendeleo na kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kujikinga na vitendo vya udhalilishaji pamoja na kuwaelimisha wanafunzi wa kike juu ya suala zima la wanawake na uongozi.

 Hata hivyo amesema kuwa maadhimisho hayo yatashirikisha wanafunzi kutoka Skuli za Unguja kutoka wilaya ya Kaskazini A, wilaya ya mjini, Wilaya ya Kati pamoja na wilaya ya Magharibi A ‘’madhimisho  hayo yataanza na shamra shamra za michezo ya aina tofauti  ikiwemo mchezo wa Mpira wa Pete (Netball), na michezo mengine itakayohusisha timu za watoto wa kike kutoka Skuli ya Tumbatu, jongowe, Mkokotoni, Mtowa pwani, Kianga, Mtoni, Kiembesamaki B na Uroa’’.  Amesema Khairat.

Kwa upande wake Rahma Ali Juma kutoka kituo Cha Mijadala kwa vijana (CYD) amesema katika michezo hiyo itahusisha pia watoto wenye Ulemavu kwani nao wana haki ya kushiriki  katika michezo kama watoto wengine .

Kilele cha madhimisho hayo kina tarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya Tarehe 12 Oktoba,2024 kwa kuanzia na mechi ya finali ya mpira wa Pete (netball) pamoja na kuoneshwa picha zilizochorwa na wanafunzi.Kauli mbiu  ya maadhimisho hayo ni "muwezeshe mtoto wa kike apaze sauti yake" 

 

 

 

 




Mhe, Hemed awapa Somo Wakaguzi wa ndani wa pewa Somo

 

Na, Asia Hakim.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema Taaluma ua Ukaguzi wa ndani ni msingi wa uadilifu na mafanikio kwa Taasisi za Umma na binafsi zinashuhulika na Taaluma hio.

Ameyasema hayo kwa niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika ufunguzi wa  Mkutano wa  Kumi na Saba (17) wa Wakaguzi wa ndani uliofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano ya Kimataifa jijini Arusha.

Amesema kutokana na  jukumu la ukaguzi wa ndani kuwa ni  muhimu kwa maendeleo ya Taifa ni wajibu wa wakaguzi wa ndani kukusanya nguvu za pamoja katika  kujenga mustakbali wenye mafanikio zaidi, usawa endelevu na utawala bora nchini.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema  kuwa wakaguzi wa ndani ni mabingwa wa utawala bora, walinzi wa uwadilifu, na ni watu wenye viwango vikubwa vya maadili hivyo huhakikisha kuwa taasisi zao  zinafanya kazi kwa viwango vikubwa, uwajibikaji, uwazi na uaminifu kwa wananchi, wafanyabiashara na washirika wa Kimataifa ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo.

Mhe. Hemed amesema Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa kudumisha uhuru na usawa wa wakaguzi wa ndani hivyo Serikali iko imara katika kuzingatia kanuni za ukaguzi wa ndani ili kuhakikisha wanafanya kazi zao bila ya ushawishi usiofaa na kutokuingiliwa katika majukumu yao ya kila siku.

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais amewahakikishia wakaguzi wa ndani kuwa Serikali inatambua na kuunga mkono kikamilifu jukumu muhimu la ukaguzi wa ndani hivyo itahakikisha inaimarisha mfumo unaowezesha kazi zao, kuongeza uwezo wa ukaguzi wa kitaaluma na kukuza utamaduni wa uwajibikaji katika Taasisi zote.

Sambamba na hayo Mhe.Hemed ametoa wito kwa wakaguzi wa ndani kuutumia Mkutano huo katika kujadiliana na kubadilishana mawazo chanya yatakayoleta uvumbuzi na maarifa zaidi katika kuendeleza Taaluma hio kwa mustakabali mwema wa maendeleo ya Taasisi zetu na Taifa kwa ujumla.

Nae Rais wa Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani Tanzania ( I I A )Dkt. ZALIA NJEZA amesema lengo la kuwepo kwa Mkutano wa wakaguzi wa ndani ni kujadiliana njia mbali mbali zitakazo wawezesha kufanya kazi zao kwa uadilifu na  uwajibikaji na  kuisaidia Serikali kufanya kazi za ukaguzi kwa  ufanisi na kwa viwango vya hali ya juu.




Dkt ZALIA amesema Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani Tanzania imekuwa na jukumu la kuhakikisha wanachama wake wanaendelezwa kielimu, kutanua wigo wa mtandao wa wanataaluma ya ukaguzi ndani na nje ya nchi pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili na uamifu ili kuisaidia Serikali katika uwajibikaji hasa wa  udhibiti wa matumizi ya rasilimali fedha.

Amesema Taasisi ya Wakaguzi wa ndani itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali zote mbili pamoja na wadau wao ili kurahisisha ufanyaji kazi kupitia taaluma  hio kwa kuwa na Wakaguzi wa ndani wenye taaluma,  ujuzi na viwango vye ubora katika ukaguzi wa ndani.

Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CPA BENJAMIN MASHAURI MAGAI amesema Ukaguzi wa ndani ni eneo muhimu endapo litaimarishwa na litaisaidia Serikali na Taasisi binafsi kuangalia rasilimali za nchi, udhibiti wa mifumo ya ndani , viashiria vya upotevu wa rasilimali na kusimamia ulinzi katika matumizi ya rasilimali kwa Taasisi zote nchini.

CPA .MASHAURI amesema  wakaguzi wa ndani nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa na  rasilimali fedha hada pale wanapolazimika kufanya kazi nje ya maeneo yao ya kazi  jambo ambali linawapa wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kwa uweledi na ufanisi zaidi hivyo wameziomba serikali kuweza kuwatatulia changamoto zinazowakabili ili kuwarahisishia ufanyaji wa kazi zao.

Akitoa salamu za Mkoa wa Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo CRISTIAN PAUL MAKONDA, Mkuu wa Wilaya ya Munduli FESTO SHEM KITEANGWA amesema Serikali imathamini jukumu muhimu linalifanywa na wakaguzi wa ndani katika kuisaidi Serikali kupiga hatua za kimaendeleo hasa katika udhibiti wa rasilimali katika Taasisi za umma na Taasisi binafsi nchini.

KISANGA amesema Mkutano huo ukawe chachu na kutoa fursa ya kusaidiana na kuendelezana kitaaluma, kubadilishana uzoefu pamoja na kuweka mikakati imara ya kufikia malengo ya Taasisi hiyo na Taifa kwa ujumla.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amekagua mabanda ya maonesho na kujionea kazi mbali mbali zinazofanywa na wakaguzi wa ndani walioshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Kumi na Saba(17) wa Taasisi ya Wakaguzi wa ndani Tanzania kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali  Mwinyi yaliyopo nje ya  Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa jijini Arusha.




“Wanawake wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi kuepuka unyanyasaji mitandaoni”

 Na.Mashavu Abdi

Wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi nchini wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi na kuepuka vikwazo vinavyyowekwa na baadhi ya watu wenye nia ya kurudisha nyuma ushiriki wa wanawake wa kufikia lengo la usawa wa 50 kwa 50 katika uongozi.

Mkurugenzi TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa ameyasema hayo katika mkutano na wadau wa masuala ya wanawake na uongozi kujadili unyanyasaji wa wanawake mitandaoni huko huko ofisi ya TAMWA-ZNZ Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Dkt. Mzuri alieleza kuwa, wakati umefika kwa wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwa kujiamini na kushinda changamoto hizo kwani wadau mbali mbali wanachukua jitihada kuhakikisha usawa wa kijinsia katika uongozi unasimamiwa na kufanya kazi ipasavyo.

‘’Kwa sasa tumepata fursa nyengine ya kuwanyanyua wanawake na kuwawekea mazingira mazuri ili waweze kujiona wako salama wanaposhiriki katika nafasi za uongozi na kufikia usawa wa 50 kwa 50", alieleza Dkt. Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA-ZNZ.

Akiwasilisha mada kuhusu rushwa ya ngono katika mkutano huo Afisa elimu Taasisi ya Kupambambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) Yussuf Juma Suleiman amesema katiba ya Zanzibar pamoja na mikataba ya kimataifa imetoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume kushiriki katika uongozi hivyo ni vyema kila mmoja kuchukuwa hatua kuhakikisha usawa katika nafasi za uongozi unapatikana.

" Kutungwa kwa sheria za kimataifa pamoja na mikataba mbalimbali ukiwemo mkataba wa Afrika wa haki za wanawake na watoto na mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake, ni moja wapo ya mifano michache ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia (rushwa ya ngono)’’ Yussuf Juma Suleiman, Afisa elimu kutoka ZAECA.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa Zanzibar Abdulrazak S. Ali amesema awali wanawake walipitia changamoto nyingi katika kugombania nafasi za uongozi zikiwemo uchumi mdogo, mfumo wa uteuzi ndani ya vyama vya siasa, ubaguzi, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na kukosa nafasi katika vyombo vya maamuzi ambapo kwa sasa changamoto hizo zimepatiwa ufumbuzi.

“Mwaka 2024 kumefanyika marekebisho makubwa ambayo yatapelekea fursa zaidi kwa wanawake kuweza kupata nafasi mbali mbali ndani ya vyama vya siasa, maboresho hayo yamezingatia jinsia na ujumuishi, kuongezwa kwa kifungu cha 10 C ndani ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2024 ambayo yatasaidia uwajibika kwa vyama vya siasa kuwa na sera ya jinsia kwa muda wote’’ ameeleza Abdulrazak S. Ali.

Kwa upande mwengine amewataka wanawake kuweka imani kwa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kwani iko mstari wa mbele kuhakikisha usawa wa jinsia unapatikana katika vyama vya siasa. 

 '' Tuwe na imani na Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwani tayari imeanzisha dawati la jinsia na kupokea kesi za masuala yanayohusiana na jinsia bila ya upendeleo na kuzipatia ufumbuzi", amesisitiza Abdulrazak S. Ali.

Akifunga mkutano huo Mjumbe wa Bodi TAMWA-ZNZ Hawra Shamte, amewaomba wadau kuelimisha jamii umuhimu wa wanawake kugombea nafasi za uongozi sambamba kukomesha vitendo vya unyanyasaji mtandaoni na rushwa ya ngono dhidi ya wanawake.

Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha wadau kutoka taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari kujadili masuala ya wanawake na uongozi ikiwemo unyanyasaji wa wanawake mitandaoni.

MWISHO

Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar

Na, Mwandisho.   Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowa...