Madakari Ngazi ya Awali Kupatiwa Elimu kuhudumia wangonjwa Mahututi

  Na.Mwandishi wetu.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema hatua ya kuwajengea uwezo watoa huduma wa vituo vya Afya vya msingi juu ya namna bora ya kutoa huduma ya awali kwa wagonjwa mahututi kabla ya kufikishwa hospitali kubwa kutaweza kuokoa maisha ya wananchi wengi nchini.

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Huduma ya Dharua na wagonjwa mahututi katika Ukumbi wa Hotel ya Verde Zanzibar.

Amesema kuwa Tafiti zinaonesha kuwa baada ya kuanzishwa mifumo ya utoaji wa huduma za dharura imesaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa vifo na vilema vitokanavyo na majanga  hivyo ni lazima  kuzidi kuimarishwa kwa mifumo hio kuanzia katika ngazi ya jamii ili kuweza kudhibiti kasi ya vifo vitokanavyo na majanaga.

Rais Dkt.Mwinyi amesema Tanzania kama nchi nyengine duniani hatuna kinga ya kutokupata dharura hasa ya majanga mbali mbali yakiwemo ajali za barabarani, baharini, vimbunga, magonjwa yasiyo ya kuambukiza na magonjwa yakuambukiza ambayo yamekuwa yakipoteza maisha au kuacha vilema vya kudumu ambavyo vinategemea msaada mkubwa kutoka kwa kada ya magonjwa ya dharura kuweza kupambana na magonjwa hayo.

Dkt. Mwinyi amesema katika kuimarisha huduma za dharura na wagonjwa mahtuti Serikali imejenga na kuzifunga hospital 10 za Wilaya na Mkoa ambazo zina miundombinu na vifaa tiba kwa ajili ya kutoa huduma za tiba za dharura pamoja na kuzindua kituo cha uendeshaji wa huduma za dharura za afya ya jamii Zanzibar chenye lengo la kubaini na kushuhulikia kikamilifu vitishio vya Afya ya jamii Zanzibar

Sambamba na hayo Dkt Mwinyi amesema Serikali imefanya ukarabati mkubwa na kuweka vifaa na mifumo ya TEHAMA katika kituo cha huduma ya dharura na Afya ya jamii (Afya Call Center) kilichopo Magomeni kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata elimu ya Afya na msaada wa haraka wanapofikwa na dharura za kiafya kwa kupiga simu bila ya malipo.

Ameupongeza Uongozi wa Akademia ya huduma za dharura (EMSA) wadau na vyama vyengine vya kitaaluma kwa kushirikiana na Serikali kusambaza huduma za dharura nchini na kuwahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango wao na inafarijika kuona juhudi zinafanyika za kuona maendeleo makubwa ya ya utoaji huduma bora ya dharura na wagonjwa mahtuti hapa Zanzibar.



Nae waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazurui amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti katika kukabiliana na majanga mbali mbali na kutokomeza kabisa ulemavu na vifo vinavyoweza kuepukika.

Mhe. Mazrui amesema kuwa uwepo wa  mifumo Imara na endelevu ya kutoa huduma ya tiba ya dharura na wagonjwa mahtuti kwa wakati kutapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto na hata majanga yatokanayo na ajali mbali mbali ambayo yanaendelea kugharimu maisha ya wananchi wengi.

Amesema licha ya uhaba wa madaktari bingwa wanaoshuhulikia utoaji wa huduma za dharura na wagonjwa mahtuti bado jitihada ya makusudi zinahitajika kutoka katika kitengo cha Imajensi na vitengo vyengine vya tiba kwa kufanya kazi kwa kushirikiana katika kutoa matibabu ya haraka kwa wananchi ili kuokoa maisha ya wananchi wengi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Akademia ya Huduma za Dharau (EMSA) Dkt. SILIVESTA FAYA amesema lengo la kuwepo kwa kongamano hilo ni kuwapatia Taaluma watendaji wa Wizara, Taasisi na Wadau wa Afya juu ya utowaji wa huduma za tiba ya dharura na wagonjwa mahtuti hasa katika ngazi ya huduma ya Afya ya msingi.

Dkt. FAYA amesema  EMSA imejipanga kuleta mageuzi makubwa ya Utowaji wa Huduma za Dharau kwa kuwajengea uwezo na kuwapatia ujuzi na vifaa tiba watoaji wa huduma hio ili kuweza kufanya kazi zao kwa uweledi na kwa wakati jambo ambalo litasaidia  kuokoa maisha ya Watanzania.


SERIKALI KUENDELEA KUTAFUTA FEDHA ELIMU YA JUU PROF MKENDA

 Na, Mwandishi wetu.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema wapo kwenye mchakato wa kuunda kamati maalumu ya kutafuta fedha kuongeza fedha za ufadhili kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi, uhandisi na elimu tiba nje ya nchi.

Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo leo Agosti 24, 2024 wakati akizindua bweni la wasichana, vyumba vya madarasa na maabara Sekondari ya Kizimkazi Dimbani ambavyo vimejengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Katika hafla hiyo, Waziri Mkenda amesema serikali inaendelea kuhamasisha wanafunzi wengi wajitokeze kusoma masomo hayo kwani hakuna taifa linaweza kuendelea kama halina wataalamu katika sekta hizo.

Amesema tayari serikali imeanzisha mfuko maalumu wa Samia Scolaship ambapo mwanafunzi katika maeneo hayo anapata ufadhili na serikali kwa asilimia 100 na kugharamiwa kila kitu anapkwenda nje kusoma.

“Kuna fursa nyingi za kusoma nje ya nchi hatuwezi kujifungia ndani kisha tukategema kuendelea hata mataifa yaliyoendela yasomesha watu wake nje, kwahiyo tuchangamkie fursa hii,” amesema

Waziri Elimu,Sayansi na Tekenolojia Prof. Adolf Mkenda (MB) akizungumza katika Uzinduzi wa Dahalia ya Waschana Kzimkazi Dimbani Ulio jengwa kwa Fedha za TASAF

“Tumeshatenga fedha lakini tunataka kuunda kamati maalumu ya kutafuta fedha kwa kushirkiana na mabenki ili kuongeza mfuko huo kuwasaidia wanafunzi kusoma,” amesema

Ametumia fursa hiyo kuwataka walimu, wazazi kuwahimiza wanafunzi kusoma masomo hayo kuanzia kidato cha kwanza ili wanufaike na fursa hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda amesema wakati wanaanzisha ofisi ya Atomu Zanzibar walitafuta watu wenye sifa lakini wamebaini kuna chngamoto kubwa ya watu wenye elimu hiyo hivyo wameanza mpango kuwekeza katika eneo hilo kuwasomesha watu wenye sekta hiyo.

Amesema wameagiza sasa itengwe bajeti katika taasisi hiyo kwa ajili ya kusomesha wataalamu hao.

“Kwahiyo mtaona kuwa kuna fursa nyingi yapo maeneo ambayo tunahitaji wataalamu lakini hatuna wa kutosha tutumie fursa hii,”

Mkurugenzi Mkuu wa Tasaf Shadrack Mzirai amesema katika kipindi cha pili cha uhaulishaji wa fedha kwa kaya masikini jumla ya Sh48.84 bilioni zimetolewa kwa kaya 53,441.

Amesema zaidi ya miradi 761 yenye thamani ya Sh15 bilioni imeibuliwa kati ya kiasi hicho, Sh1.98 bilioni zimetumika kununua vifaa huku Sh13 bilioni zikitumika kulipa ujira kwa wananchi wanaoshiriki kujenga miradi hiyo ambao wanatokana na kaya hizo zinazonufaika na mfuko.

“Katika miradi iliyoibuliwa ni pamoja na barabara, ujenzi wa shule, mazingira uvuvi na miundombinu hivyo wananchi hao kujiongezea kipato kile kinachotokana na mfuko wenyewe.




Amesema kupitia mpango huo wamenzisha vikundi vya ujasiriamali mbapo zidi ya wananchi 23, 000 wamenufaika.

Amesema Tasaf imeunganisha kanzi data Bodi ya Mikopo kuwasaidia wanufaika wa Tasaf ambapo wengi wameendelea kunufaika

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Abdalla Said amesema vyumba vinne vya madarasa vyenye uwezo wa kubeba wanafunzi 180 sawa na wastani wa wanafunzi 45 kila darasa.

Kwa mujibu wa katibu Mkuu maabara na vyumba hivyo vimegharimu zaidi ya Sh400 milioni.

Hatahuvyo amesema Serikali inaendelea kuhakikisha inaondoa changamoto za elimu na wanafunzi wasisome mikondo miwili.


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na Uongozi wa TASAF

 

Na, Mwandishi wetu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amewataka watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya wananchi zinalindwa na kutumika ipasavyo ili Watanzania waendelee kunufaika na Mfuko huo

TASAF uliofika Ofisini kwake Vuga  kwa lengo la kujitambulisha.

Amesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya jamii  TASAF umekuwa ni mkombozi kwa Watanzania walio wengi hasa wanyonge hivyo uongozi huo una jukumu kubwa la kuhakikisha unadhibi na kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za mfuko huo.




Makamu wa Pili wa Rais ameutaka Uongozi huo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF  SHEDRACK MZIRAY   kulipa kipaombele suala la utoaji wa Taaluma kwa wanufaika juu ya Dhamira na Malengo ya mfuko huo ili kupunguza malalamiko kwa wanufaika hao mara tu wanapomaliza ama kukosa sifa za kuendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na TASAF.

Aidha Mhe. Hemed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoka mashirikiano  makubwa kwa watendaji wa TASAF wa Pande zote mbili za Muungano ili kuhakikisha Watanzania wanaendelea kunufaika na mfuko huo na malengo ya Viongozi wakuu wa Serikali ya kuwaondolea changamoto mbali mbali wananchi wake yanafikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndugu SHEDRACK MZIRAY amesema atahakikisha anayafanyia kazi  maelekezo na maagizo yote waliyopatiwa na  Makamu wa Pili wa Rais kwa kuendelea kudhibiti Nidhamu katika matumizi ya fedha, Nidhamu kwa watendeji wa mfuko huo na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya kuwepo kwa mfuko huo nchini.

MZIRAY amesema Tasaf imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na kwa mashirikiano mkubwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hivyo anaamini kuwa  ushirikiano huo utaendelea  kudumu katika kipindi chote cha Utumishi wake na kuahidi kuwa Matunda ya Mfuko huo yatawafikia na kuwanufaisha wananchi  wa pande zote mbili za Muungano.



Jamii ya Shauriwa kutunza Mazingira ili kurithisha Vizazi vijazo

 


  Na, FATMA  RAJAB


Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo umwagiliaji  maliasili na mifugo zimeanzisha mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijani (The Green Legacy Zanzibar) lengo ikiwa ni kuifanya  Zanzibar kubaki  katika hali yake ya ukijani wa asili.

Hayo yameelezwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman. katika uzinduzi wa mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijani uliofanyika Nyamanzi mkoa wa magharibi Unguja.

Alisema kupitia hali ya kijani  Serikali ilianzisha mipango ya kupanda na kuhifadhi miti tangu mwaka 1964 pamoja na kuendeleza juhudi mbali mbali zilizochukuliwa miaka ya nyuma za kuhifadhi misitu.

Aidha, alisema mpango huo unakusudia kuwashirikisha na kuwaleta pamoja wadau mbali mbali kutoka sekata na ngazi zote kupanda na kuitunza miti ya aina zote.

Aidha alisema kuwa, mpango huo una kusudia kuongeza hamasa kwa kila mtu kushiriki kikamilifu pamoja na kujenga jamii yenye utamaduni na tabia endelevu ya kuthamini, kupanda, kutunza miti na kuepuka kukata miti ovyo ili kuepusha athari mbali mbali ambazo zinaweza kujitokeza kwa kukatwa kwa miti.

Mhe, Makamu alisema kuwa, mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijani umekuja mara baada ya kuona kuwa kumekuwepo  na mambo mengi ambayo  yanasababisha  upoteaji mkubwa wa miti na misitu  kutokana na shughuli mbali mbali za kibinaadamu  pamoja na ukuaji wa miji ambayo ujenzi wake unachukuwa eneo kubwa  la ardhi Kutokana na  ongezeko la idadi ya watu pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Sambamba na hayo alisema mpango huo pia umeanzishwa kuhsmasisha na kuwawezesha wananchi wa Zanzibar pamoja na watu mbali mbali  kuelewa umuhimu wa misitu na kuihifadhi miti iliyopo kuipanda na kuitunza ili kuimarisha mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.


Nae, waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda Mhe, Omar Said Shaabani. alisema mpango wa uhamasishaji upandaji wa miti katika jamii ni sehemu ya misha ya viumbe hai hivyo jamii inatakiwa iwe na utamaduni wa kuyaenzi na kuyatunza mazingira kila wakati kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

"Tutaendelae kushirikiana vizuri na wizara ya elimu na mfunzo ya amali ili kuhskikisha kuwa wanawafundisha wanafunzi wa Sekondari na vyuo vikuuu kujua umuhimu na thamani ya upandaji wa miti kuweza kufikia dira ya mpango huo.

Kwa upande wake Mstahiki meya Mhe, Mahmoud Mohammed Mussa. ameeleza kuwa serikali kupitia youth climatic fund imezitaka Taasisi na mashirika mbali mblia kwa ujumla na kuhamasisha utunzaji wa miti na kutunza mazingira muda wote."mpaka sasa tumepanda miti isiyopungua elfu kumi kwa upande wa visiwa vya unguja na pemba ambapo mradi wa youth climatic umefikika katika ushindani wa kutafuta vikundi vitakavyofanya kazi katika kuwezesha upandaji wa miti elfu tatu. 3,000,000.

Mpango huo utainufaisha jamii ya Zanzibar kwa kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi na hasara nyengine za kimazingira, ambao umekuwa na kaulimbiu isemayo "Zanzibar ya kijani inawezekana shiriki kupanda na kutunza miti".


Wajasiariamali wa TASAF waishukuru Serikali Kushiriki Maonesho ya Kilimo Dole.


 Na, Mwandishi wetu

Wajasiriamali wanaonufaika na mradi wa maendeleo  ya Jamii TASAF wameishukuru serikali  ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia mradi wa Tasaf kwa kuwawezesha  kushiriki maonesho ya nane nane  yanayoendelea Dole wilaya ya Magharibi A ambayo yamewaongezea fursa mbalimbali za kiuchumi na Biashara.

Wametoa kaulihiyo Mapema leo huko Dole wakati walipokuwa wakifanya mahojiano na kueleza mafanikio waliyoyapata kutokana na uwepo wa maonesho hayo ya nanenane ambayo yametoa fursa ya kuuza bidhaa Zao na kujitangaza kibiashara.

Akitoa Ufafanuzi juu ya ushiriki wa walengwa hao wa Mpango katika Maonesho hayo Afisa Ufuatiliaji Zanzibar, Ramadhani Madar. amesema kuwa  TASAF imekuwa ikwashirikisha walengwa kutoka Unguja na Pemba katika Maonesho mbalimbali kwa lengo la kujitangaza na  Kuuza Bidhaa  wanazo zizalisha ili kupata Masoko na kujiendeleza kiuchumi.

Madari ameeleza kuwa, Lengo la TASAF ni kuwatafutia Masoko  ya Kuuza Bidhaa Mbalimbali  wanazo zizalisha kupitia vikundi vyao  ambavyo vimekuwa msada mkubwa wakupata maendeleo na kufikiwa lengo la TASAF.

wajasiriamali wa TASAF wakiuza Bidhaa zao kwa wageni katika Maonesho ya nanenane Dole 

Aidha wajasirimali hao wamesema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia TASAF imekuwa ikiwawekea mazingira wezeshi ya Kushiriki maonesho ambayo yamekua chachu ya kupata masoko ya Bidhaa zao. ameleza Mzee Hassan.

Ameeleza kuwa, kwa sasa nimefikia ukomo wakuwa mwanakaya lakini naishukuru serikali kwakuniwezesha  kuendesha maisha yangu kupitia fedha za TASAF na kupitia biashara ndogondogo tunazo ziendeleza.

Kwa Upande wake Bi.Mariayam Kassim Abdallah. amesema uwepo wao katika maonesho hayo wamepata kujifunza namna ya kutengeneza  bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali wengine jambo ambalo limewafanya kuzitangaza biashara zao kwa wananchi wengine kwa Urahisi.

Nae, Raya Sulieman Hamadi, kutoka Kaskazini pemba ambaye ni mnufaika wa TASAF ameeleza kuwa amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na TASAF kuwapeleka katika Maonesho kama hayo amabayo yamekuwa na Msada mkubwa kibiashara.

Moenesho hayo ya nane nane ambayo ni ya saba yenye kauli mbiu ya ‘’Kilimo ni utajiri kila Mtu atalima’’ yanatarijiwa kufungwa kesho katika viwanja hivyo vya Dole .


Wananchi wa Shauriwa kuunga Mkono juhudi Za Serikali Kutunza Miundombinu

 


 Na, Mwandishi wetu

Jamii imeshauriwa kuunga Mkono jihudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi katika  sehemu mbalimbali  nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe, Hamza Hassan Juma  ametoa kauli hiyo Kizimkazi Dimbani wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jmaii TASAF Kwa Upande wa Zanzibar.

Amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  ndio waratibu na wasimamizi wa miradi mbalimbali ya Muungano ambayo inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jmaii TASAF  ambayo imekuwa ikisaidia wananchi  katika maeneo mbalimbali ya nchi

Alisema kuwa, Miradi ya elimu, Afya na ujenzi wa Miundombinu ya Barabara imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya wananchi hivyo nivyema wananchi kupitia maeneo yao kuitunza na kuiendeleza miradi hiyo ili iweze kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, Waziri Hamza. ameendelea Kuwaasa wananchi na wahusika wa Miradi hiyo  kuenedelea kuitunza kwani miradi hiyo imeharimu fedha nyingi za Serikali na inanufaisha wananchi wengi kwawakati mmoja.

Akizungumza katika Ziara hiyo mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji. ameeleza kuwa Miradi hiyo imeharimu fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kwenda kwa wananchi.

Ameeleza kuwa jumla ya Tsh  215,000,000.zimetumika katika  ujenzi wa kituo cha Afya Upenja, na jumla ya Tanzania Tsh 117,000,000.zimetumika katika ujenzi wa  ukumbi wa mkutano  Skuli ya Bambi huku jumla ya Tsh  291.1 zimetumika katika Ujenzi wa  Dahalia ya wanawake Skuli ya Kizimkazi Dimbani.

Katika hatua nyengine mratibu  ameeleza kuwa miradi hiyo ambayo imejengwa kwa mashirikiano makubwa kwa nguvu za wananchi inakaribia kumalizika na kukabidhiwa kwa sekta husika kama ilivyo kubaliwa katika sheria.

Kwa Upande wake muhandisi kutoka wizara ya Afya  ameleza kuwa miradi hiyo imejegwa kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya wanachi na tayari imefikia aslimia 75% kukamilika kwa wakati ulio pangwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Mzee Ali Mohamed Mrisho. mkaazi wa Bambi alieleza kuwa wanafurahishwa na kuridhishwa na kazi inayofanywa na Serikali zote mbili katika utekelezaji wa maradi na ujenzi wa ukumbi wa Mitihani katika eneo loao ambapo kabla yahapo walikuwa  wakipata tabu kuwaweka wanafunzi kufanya mitahani katika darasa moja.

jumla ya miradi mitano imetembelewa katika ziara hiyo ikiwemo kituo cha Afya upenja,ujenzi wa ukumbi wa mitihani Bambi, Ujenzi Dahalia ya wanawake kizimkazi Dimbani ,ukarabati wakituo cha Afya kwa Mtipura pamoja na Ukarabati wa Skuli ya maandalizi Mkele.


Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar

Na, Mwandisho.   Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowa...