Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kufanyakazi na Sekta Binafsi

 

Na,Mwandishi wetuu.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na Taasisi binafsi kwa lengo la kuwaondoshea wananchi changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika katika Kiwanja cha Ofisi ya Sheha wa Shehia ya Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na  Taasisi Binafsi ikiwemo Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation ( MIF ) iliyolenga kupambana na ujinga, maradhi na umasikini hasa kwa wanawake na watoto.

Mhe. Hemed ameipongeza Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation kwa kuendelea kuisaidia Serikali kupitia Sekta mbali mbali kama vile Elimu, Afya, Uwezeshaji na nyenginezo kwa  lengo la kumsaidia mwananchi hasa mwanamke kujikwamua kiuchumi na kumuwezesha kuweza kujitegemea.

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefurahishwa kuona katika maadhimisho hayo shughuli mbali mbali za kijamii zitafanyika ikiwemo uchangiaji wa damu salama itakayosaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto, vifo vitokanavyo na ajali na majanga mbali mbali yanayohitaji damu salama na kwa haraka zaidi.

Sambamba na hayo amewakumbusha na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuitunza amani na umoja uliopo nchini ambazo ndizo nyenzo muhimu ya kufikia maendeleo ya Serikali iliyojiwekea kwa waanchi wake.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Afya wa Zanzibar, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Riziki  Pembe Juma ameipongeza Taasisi ya MIF kwa kuendelea 


kuekeza katika harakati za maendeleo hasa katika kumuinua Mwanamke kiuchumi, kuimarisha Afya ya jamii na kuokoa vifo vya mama wajawazito na wahanga wa majanga mbali mbali.

Mhe. Pembe amesema Taasisi ya MIF imekuwa mstari wa mbele kujitoa katika kupambana na changamoto mbali mbali zinazokwamisha maendeleo nchini na kuhakikisha mwanamke wa Kitanzania anapata fursa mbali mbali za kimaendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation Mhe. WANOU HAFIDH AMEIR amesema lengo la kufanyika kwa matembezi ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia ni kuwashajihisha wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha Afya na kupambana na maradhi nyemelezi ambayo yamekuwa yakienea kwa kasi nchini.

Amesema Taasisi ya MIF Imejipanga kupambana na adui maradhi, umasikini na ujinga kwa kuhakikisha inawafikia Watanzania popote walipo katika kuwawezesha kupambana na maadui hao kwa maendeleo ya Taifa.

Mhe. Wanu amesema kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni "MOYO WANGU MAISHA YANGU" inayolenga kuwafahamisha wananchi kutunza afya zao dhidi ya maradhi yasiyoambukiza yakiwemo kisukari, sindikizo la damu na maradhi ya moyo  pamoja na kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya Watanzania wanaopatwa na majanga mbali mbali.

Katika maadhimisho hayo ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais Dkt. Samia Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation imetoa msaada wa gari nne (4) za kubebea wagonjwa (Ambulance) mbili kwa hospitali za  Unguja na gari mbili zitapelekwa Pemba  pamoja na viti hamsini (50) kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum na kuwaomba wahusika kuvitunza vizuri vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu .

 

 

 

 

 




Wajasiriamali wa TASAF waeleza Mafanikio ya Mpango huo Zanzibar



Na, Mwandisho. 


Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameeleza namna mpango huo ulivyowaondoa kuitwa kaya masikini na sasa wanaweza sio tu kujitegemea bali wamekuwa msaada kwa watu wengine.

Mpango wa kunusu kaya masikini kwa Zanzibar ulianza mwaka 2013 ukiwa katika afua tatu: Ruzuku, ajira za muda na miundombinu ambapo mpaka sasa ina vikundi 3,372 vyenye wanachama 45,948.

Vikundi hivyo vimekusanya akiba ya zaidi ya Sh1.6 bilioni na vimeendelea kukopeshana kwa ajili ya kuanzisha na kutekeleza miradi ya kuwaongezea kipato.

Wakizungumza katika maonyesho ya biashara ya kimataifa Dimani Nyamanzi Januari 13 2025, baadhi ya wajasiriamali wanaonufaika na mfuko huo wamesema hawakuwahi kufikiria kama wanaweza na wao wanweza kushirkia maonyesho makubwa ya biashara kama hayo.

Khadija Slaym Salim mkazi wa Kianga amesema mwanzo walikuwa kaya masikini lakini kwasasa wanajivunia kunufaika wamenufaika kupitia kwenye vikundi vyao na kujiongezea vipato.

“Ukiachilia mbali kuwa kwenye vikundi lakini kila mtu nyumbani kwake anaedesha biashara zake binafsi mimi nyumbani ninamlango wa duka kila ninachopata naongeza, Tasaf imetunufaisha tunaweka akiba ikifika mwisho wa mwaka tunagawana zingine tunaacha kuendeleza biashara zetu,

Khadija mesema mbali na kunufaiaka mmojammoja lakini wamenufaika kwenye huduma za kijamii kama shule, barabara, na hospitali kwasasa watoto wanakwenda shuleni bila changamoto zozote



“Tofauti na mwanzo watoto walikuwa wanashindwa kwenda shule, mikoba ya daftari hawakuwa nayo, mtoto akienda shule tulikuwa tunakunguta mifuko ya unga tunawapa lakini sahiv begi wanapata,” amesema

Amesema huu mpango walioleta umesaidia wanawake kwani kipindi cha nyuma ilikuwa lazima mpaka wategemee wanaume lakini kwasaa wanajitegemea wenyewe na kuwasaidia wengine.

Ametumia fursa hiyo kuwasihi wanawake wanapopata fursa kama hiyo kijiendelza kwenye vikundi ili wazidi kujikwamua kimaisha.

 

Mnufaika mwingine, Naomba Bakari Hassan kutoka Kikundi cha Kutoa ni moyo Chakechake Pemba amesema walikuwa na maisha magumu lakini kwasasa wanaendelea kuimarika kupitia kwenye vikundi vyao.

“Sasahivi tunasomesha watoto tunapata fedha za huduma za nyumbani na kusomesha watoto tofauti na ilivyokuwa awali tunashukuru tunapata kwasaa tumeondoka kwenye utegemezi, kwasasa kila kitu tunaweza kufanya wenyewe na tumeimarika,” amesema Naomba

Amesema kabla ya kuingia kwenye mradi alikuwa na maisha magumu lakini kwasasa ni maisha bora, “familia yangu inakula, namimi najitosheleza mahitaji yangu kupitia biashara ninayoifanya.

Naomba anayefinyanga viotezo na kushona mikoba anasema ndoto zake anataka awe mfanyabiashara mkubwa na kuwa na maisha bora zaidi.

Mwingine mtoto wa mnufaika Raya Suleiman Hamad kutoka kukindi Tushikamane cha Mgogoni Wete Pemba anasema wazazi ndio wapo kwenye mpango walipopata ruzuku wakatengeneza mafuta na bidhaa zingine kwa ajili ya kuuza.

Raya ambaye amesomeshwa na ruzuku ya Tasaf iliyokuwa ikitolewa kwa wazazi wake, amesema kwasasa ameshakuwa mtaalamu kwenye ujasiriamali baada ya kufundishwa hivyo wanataka kufika mbali zaidi kwenye maisha.


Mkurugenzi wa Mifuo na Mawasiliano ya Umma Tasaf, Japhet Boaz amesema hizi zilikuwa kaya masikini ambazo hazikuwa na uwezo kujitokeza ila kwasasa wameugana pamoja na wanatengeneza bidhaa na kuja kwenye maonesho kama haya ya kimataifa.

“Wametumia faida kuwapeleka watoto shule, na kujiwekea akiba wakifanya mambo mengi ya maendeleo na kuimarisha makazi yao na kuwekeza mengine,” amesema

Kwa mujibu wa Boaz, wanatiwa moyo kwamba kazi wanayoifanya na kazi ambayo serikali imedhamiria kwa wanachi wake inaleta matunda.

Amesema kaya baada ya kuzisaida wanaziweka kwenye vikundi, wanaweza kuweka akiba na wanaweza kukopeshana eneo ambalo nalo linafanya kazi vizuri.

“Kiasi kwamba hata hawa tunaowaona hapa kwenye maonyesho wametoka kwenye vikundi wakabuni miradi kulingana na mazingira waliyonayo kisha wameendelea kutengenza vitu mbalimbali na bidhaa nyingi zinazotokana na asili,” amesema

Kwa upande wa Zanzibar kuna afua tatu, wanatoa ruzuku ya fedha kwa kaya masikini ambapo mpaka sasa wameshatoa Sh50.1 bilioni kwa muda wa miaka 10 kwenda kwenye kaya masiki.

Afua ya pili wanatoa ajira za muda kwenye kaya hizo ili kuwaongezea kipato wanabuni miradi katika jamii wanafanya kazi wanapata ujira unaowasadia kuongeza kipato.

Afua nyingine ni ujenzi wa miundombinu ambapo katika hilo wanaangalia eneo ambalo linapungukiwa katika sekta ya elimu, afya pamoja na maji.

Amesema Tasaf imekuwa mstari wa mbele kuitikia wito wa serikali ambapo katika sherehe hizi za Mapinduzi wamezindua vituo vya afya viwili, Upenja Kaskazini Unguja ambachokitahudumia zaidi ya wananchi 1100 na Kingine kipo Wete Pemba Kinyikani na nyumba ya watumishi.

Amesema wameona kuna upungufu wa huduma za jamii kwahiyo kaya masikini wanazohudumia inakuwa ni ngumu kufuata huduma hizo kwahiyo inawaletea athari kubwa.

Amesema wanaamini kaya nyingi pamoja na jamii nyingine watapata huduma katika maeneo waliopo kwa ufanisi zaidi.

Naye Mratibu wa Tasaf Unguja, Makame Ali Haji amesema kwa taratibu za Tasaf kila kikundi kinakuwa na wanachama 15 ambao wanajiweka pamoja kujiweka akiba na kuanzisha biashara ndogondogo, “tunashukuru wametumia rasimali za bahari kujiendeleza kiuchumi”

“Wapo wanaolima mwani na wengine wameanzisha uzalishaji wa sabuni unaotokana na mwani, tunashukuru sana wananchi hawa wameweza kujiimarisha kiuchumi na tunafahamu mpango huu unaendelea vizuri,” amesema Makame

Amesema walengwa hao ni kwamba wametoa katika mpango wa masikini na kutafuta wengine wapige hatua wajiendeleze na kujikwamua kiuchumi.





.


JAFO AFUNGUA MAONESHO YA KUMI NA MOJA YA BIASHARA ZANZIBAR




NA, Fatma Rajab  



Waziri wa viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Suleiman Said Jafo amesema maonesho ya 11 ya biashara ni jukwaa muhumu la ukuzaji wa sekta ya biashara na uwekezaji nchini.

Akifungua maonesho ya 11 ya biashara Zanzibar huko Nyamazi alisema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata taarifa mbali mbali za kibiashara hali inayopelekea ukuaji wa biashara na uchumi na uwekezaji nchini.

Katika kuboresha maonesho hayo Waziri Jafo aliziomba Wizara husika kuhakikisha inajenga majengo ya kudumu katika maonesho hayo ili kuweka mazingira mazuri ya maonesho hayo.

Katibu mkuu wizara ya maendeleo ya viwanda na biashara Zanzibar bi Fatuma Mbarouk alisema maonesho hayo tangu yalipoanzishwa  mwaka 2014 yamekuwa chachu ya ukuaji wa biashara nchini  kutokana na kuengezeka kwa wafanya biashara mwaka Hadi mwaka

Mapema Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara Zanzibar Ali Suleimani Amour aliiomba serikali kuhakikisha kua kampuni binafsi zinapewa fursa za kuandaa maonesho makubwa kama hayo ili kutoa fursa ya ushindani mkubwa wa kibiashara nchini.

Maonesho hayo ambayo yanabeba kauli mbiu ya biashara mtandao kwa maendeleo ya uchumi na uwekezaji yameshirikisha wafanya biashara kutoka sekta mbali mbali za kibiashara wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania




 

ZSTC yaridhiishwa na Chuo cha Mafunzo Katika Uimarishaji wa Zao la Karafuu

  Na. Mwandishi Wetu. Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Nd. Soud Said Ali amesema Shirika la Biashara Z...